Waziri Nape Nnauye: Miamala ya simu kutungiwa Sheria iwe 'Dhamana ya Mikopo Benki'

Waziri Nape Nnauye: Miamala ya simu kutungiwa Sheria iwe 'Dhamana ya Mikopo Benki'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Serikali imeeleza kuwa ongezeko la matumizi ya miamla ya fedha kwa njia ya simu imewapa wazo la kutunga sheria kutambua njia hizo zitambulike ikiwezekana kwa kuangalia uchumi wa mtu na itumike kama dhamana wakati wa kukopa benki.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hayo leo Aprili 6, 2022.

“Huduma ya kifedha za mawasiliano ya simu ya mkononi imekuwa mkombozi hasa kwa wale ambao huduma za benki hazijawafikia hasa vijijini na kumekuwa na ongezeko la matumizi kuliko hata benki kwa baadhi ya maeneo,” - Nape.

Soma: Mazingira ya Kisheria na Kifedha kwa Biashara Ndogondogo Nchini Tanzania
 
Serikali imeeleza kuwa ongezeko la matumizi ya miamla ya fedha kwa njia ya simu imewapa wazo la kutunga sheria kutambua njia hizo zitambulike ikiwezekana kwa kuangalia uchumi wa mtu na itumike kama dhamana wakati wa kukopa benki...
Ukisikia Digital Development, maendeleo ya kidigitali, ndio haya,

Naunga mkono hoja.

P
 
Kuumbe ndio maana lochi tamuu akanunua goti

Jamaa alichungulia fursa.
 
Fomeni wa ujenzi anatumiwa fedha na kibosike mwenye mjengo alipie gharama za ujenzi. Huyu lazima mianala yake itaonesha yuko vizuri. Mkopeshe uone ndio utajua kumbe alikuwa anazungusha fedha za mwenyumba. Benki wana akili kuliko huyu mheshimiwa hawatakubali kuchezea deposits za wateja wao.
 
Mi sajaelewa yani kama ninamiamala mingi ya mpesaniruhusiwe kukopa Crdb bila hati ya nyumba

ama au iyo miamala iwe ndo statement ya kuonyesha uwezo wangu wa kulipia

Ama Timiza iboreshwe?
 
Serikali imeeleza kuwa ongezeko la matumizi ya miamla ya fedha kwa njia ya simu imewapa wazo la kutunga sheria kutambua njia hizo zitambulike ikiwezekana kwa kuangalia uchumi wa mtu na itumike kama dhamana wakati wa kukopa benki...

Hakuna kitu kama hiki na haitowezekana
 
Mi sajaelewa yani kama ninamiamala mingi ya mpesaniruhusiwe kukopa Crdb bila hati ya nyumba

ama au iyo miamala iwe ndo statement ya kuonyesha uwezo wangu wa kulipia

Ama Timiza iboreshwe?
🤣🤣🤣🤣, kama Mo aligoma kumkopesha Kigwa na ana financial stability... ndio benki ziriski kwa kwa miamala ya simu...

Ndege wafananao huruka kundi Moja, sio kosa lake shida bosi wao
 
Sasa tukiingia huko, rasmi, BIG BROTHER WILL WATCH US 24/7! Track us! Trap us!
Kimaandishi ni zuri. Je, kivitendo ndiyo itatendekaje!?
 
Elimu Siyo Cheti, Ni Ujuzi Wa Kung'amua Mambo
 
Back
Top Bottom