Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri Nape ametoa kauli hiyo tarehe 16 Julai, 2024 mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Kisharara, Kata ya Karambi wilayani Muleba, mkoani Kagera akiwa katika siku ya pili ya ziara yake kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
"Wito wangu kwa wananchi moja watumie hizi huduma, kwa sababu kadri idadi yao inavyoongezeka inatusaidia kuona namna ambavyo gharama zitapungua lakini pia tunaupa thamani mradi huu, fedha iliyolazwa hapa (zaidi ya milioni 300) kama watumiaji watakuwa hawaongezeki inakuwa hasara kwa watoa huduma na kwa Serikali".
Waziri Nape ameipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kujenga minara imara na yenye uwezo mkubwa na kuitaka kuongeza nguvu ya kukopesha wanavijiji simu ili kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hizo.
Awali akizungumza na Viongozi wa Mkoa, wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na watoa huduma katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Waziri Nape amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi mkoani humo kusimamia ipasavyo kodi ya pango katika maeneo yote yaliyojengwa minara kwenye ardhi ya kijiji ili iwe na matokeo chanya na wananchi wanufaike na ardhi yao.
"Mheshimiwa Waziri mnara huu umeshatoa ajira kwa mawakala saba na mzunguko wake tangu tumewasha mnara ni shilingi milioni 25 hadi 50, vilevile tumetoa ajira za muda mfupi kwa wajenzi ambao ni watu wanaotoka hapa hapa kijijini na ajira ya muda mrefu kwa Mlinzi,"
Waziri Nape pia amekagua minara katika Kijiji cha Kasharara, Kata ya Karambi Wilaya ya Muleba na Kijiji cha Katahoka Kata ya Katahoka Wilaya ya Biharamulo.