Waziri Ndalichako, naona kama Elimu haiendeshwi naye bali inajiendesha yenyewe

Mzazi ashindwe kumpeleka mtoto wake shule za maana kama FEZA,CANOSA etc aje asumbue watu jukwaani hapa.
.......majitu kama hayo kutwa kupigia debe serikali ya CCM....
 
Mwanachi wa kawaida hawezi akapeleka lawama kwa rais badala ya wizara husika.

Kufanikiwa kwa wizara sifa zinamwendea waziri husika hivyo hivyo kufeli lazima waziri alaumiwe
 
Mzazi ashindwe kumpeleka mtoto wake shule za maana kama FEZA,CANOSA etc aje asumbue watu jukwaani hapa.
.......majitu kama hayo kutwa kupigia debe serikali ya CCM....
Ccm ni kichaka cha madhira ya watanzania
 
Ndalichako ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri? Hivi unafahamu namna nchi inavyoendeshwa?

Huna hoja ya yenye mashiko ya kumtaka Prof. Ndalichako ajiuzulu.

Hizo shule za kata kupata ziro zimeanza leo?
soma vyema uelewe nimeitaja na serikali. yeye alitakiwa aweke mipango hata ya kuishauri serikali kuweka part time ili angalau kuweka uwiano . serikali inapenda mipango
 
Anaitwa PROFESA!Usisahau.
 
Shule kama Mzumbe,Kibaha,Feza hata usiwe na mwalimu hata mmoja bado watu watapiga one darasa zima.
Hakuna mwalimu wa kumfanya mwanafunzi apate A kwa nature ya elimu ya Tanzania......labda kwa shule zinazoiba mitihani
Hizo one watazipiga jee kama hamna walimu wa kuwafundisha.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Tunapata tabu kuajiri walim wengine kwa sabab ya mirad mikubwa tulioanzisha- stiglier, jnhpp... ukweli ni kwamba Kuna upungufu mkubwa wa walim shule za sekondari hasa masomo yanayo kimbiwa na wengi- sayans
 
Hivi Yule rasta anafundisha lugha Magomeni anaitwaje?
 
Ndalichako amepwaya kwenye hyo wizara, kiasi Ummy Mwalimu amekuwa ka Waziri wa elimu, Ndalichako anahitaji kupumzishwa
Akili gani hii!

- Unataka Ndalichako awe mwalimu wa hisabati?

- Unataka Ndalichako ndie aajiri walimu wakutosha kufundisha hesabu?

Haya mambo ni suala la sera inayoendana na utimilifu wa bajeti, kama serikali kuu inajua kuna upungufu wa walimu shule nyingi za serikali kila mwaka, kwanini wasitenge fungu la kutosha kuajiri walimu?

Siku hizi wizara nyingi hazipewi bajeti wanazohitaji panakuwa na upungufu na matokeo yake ndio haya, hilo sio kosa la Ndalichako.

Hizi akili zenu za kukariri ni janga la taifa.
 
Ndalichako ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri? Hivi unafahamu namna nchi inavyoendeshwa?

Huna hoja ya yenye mashiko ya kumtaka Prof. Ndalichako ajiuzulu.

Hizo shule za kata kupata ziro zimeanza leo?
Hebu nisaidieni, shule za msingi na sekondari kweli ziko chini ya Wizara ya Elimu au Tamisemi
 
Hebu nisaidieni, shule za msingi na sekondari kweli ziko chini ya Wizara ya Elimu au Tamisemi
Ziko chini ya TAMISEMI. Wizara ya elimu inahusika kwa sera tu.
 
ndio maana nimetaja na serikali. lakini kama mtu anakukabidhi watoto wake uwasimamie wale na wavae kama hatoi chakula nguo wewe utasimamia vipi kula na kuvaa kwao. hapo ni kujiudhuru na kusema nimeshindwa kusimamia vitu ambavyo havijakamilika. kuliko kudanganya watu kuwa unasimamia. kuna nchi umeme ulikatika kwa muda mfupi tu waziri akajiuzuru haijailishi ulikatika kwann yanaangaliwa madhara unawezaje kuongoza au kusimamia kitu kisichokamilika.
1 awaambie walimu wafundishe kwa uwiano wa mwalimu moja wanafunzi kadhaa iwe ni amri asidishe.

maana inawezekana wanaohusika na kuajiri hawajui uwiano.

2.kuwe na mgomo mpaka mwajiri aajiri
 
Mleta mada pole Kwa maumivu unayoyapata kuhusu watoto wa kitanzania! Unaikumbuka Ile slogan ya watanzania kuitwa wanyonge?
Watanzania Hawa walioitwa wanyonge ndio wapiga kura wa ccm na ili uwe kundi la wanyonge hao lazima isiwe na elimu!
So, sera ya elimu Kwa ccm siyo kipaumbele.
Kipaumbele Cha ccm ni kuwaandaa wajinga wengi ambao watakuja kuwa wapiga kura wao baada ya kubatizwa na kuitwa wanyonge! Tafakari utanipa kongole baadae!
 
Shule kama Mzumbe,Kibaha,Feza hata usiwe na mwalimu hata mmoja bado watu watapiga one darasa zima.
Hakuna mwalimu wa kumfanya mwanafunzi apate A kwa nature ya elimu ya Tanzania......labda kwa shule zinazoiba mitihani
Kumbuka wanafunzi wa shule ulizozitaja ni Fast learners tunaziita special schools wanaozungumziwa hapa ni medium and slow learners ndo waliobaki shule hizi za kawaida ,ratio inayotakiwa ni mwl mmoja wanafunzi 40 ,sasa wanafunzi zaidi ya 1000 kwa walimu wawili wapi na wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…