The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza kusimamishwa kazi kwa Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni kutokana na kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi katika eneo hilo.
Ametoa agizo hilo Februari 20, 2025, wakati wa ziara ya Waziri Ndejembi katika Wilaya ya Handeni, ambapo alitembelea eneo la Kwanjugo Kitalu A. Wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu kuchukuliwa mashamba yao bila kulipwa fidia stahiki.
“Hili eneo lina historia yake na lina wamiliki wa asili. Haiwezekani wananchi waendelee kuonewa kwa sababu ya uzembe wa watendaji wa serikali. Migogoro hii inatokea kwa sababu hatuwasikilizi wananchi wetu. Hivyo, namuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara kumsimamisha mara moja Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri na kuteua mtaalamu mwingine atakayekuwa na uwezo wa kutatua changamoto za ardhi katika Handeni,” alisema Mhe. Ndejembi.
Aidha, Waziri ameagiza kuundwa kwa timu maalum ya uchunguzi itakayokuwa chini ya Kamishna wa Ardhi. Timu hiyo itafanya tathmini ya umiliki wa viwanja vya eneo hilo ndani ya wiki moja na kubaini iwapo kuna watumishi wa ardhi waliohusika na unyang’anyi wa ardhi ya wananchi.
“Hatutaruhusu vitendo vya watumishi wa umma kunyang’anya ardhi ya wananchi. Timu ya uchunguzi ije hapa Handeni na ituletee ripoti ya kina ili hatua kali zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika,” alisisitiza Waziri Ndejembi.
Hatua hii inakuja kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kutatua migogoro ya ardhi nchini na kuhakikisha haki za wananchi zinalindwa ipasavyo.