Waziri Ndejembi aagiza shamba la mjane kurudishwa, aonya wavamizi wa ardhi Dodoma

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG-20250426-WA0038.jpg

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Geofrey Mwamsojo kumrudishia shamba lake, Bi. Madina Hassan kutoka kwa Moses Kabeja anaetajwa kulimiliki bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Mhe. Ndejembi ametoa agizo hilo mara baada ya kufika katika shamba hilo lililopo eneo la Msalato jijini Dodoma kufuatia malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa Bi Madina ambaye alieleza kuwa shamba lake lilikua linatumiwa pia na Bw. Kabeja.

“ Baada ya kupitia nyaraka zote na kusikiliza pande zote mbili ikiwemo majirani, nimejiridhisha kuwa shamba hili ni la Mama huyu mjane, hivyo nakueleza kamishna msaidizi wa Dodoma kurudisha eneo hili kwa Mama huyu ambaye ndiye mwenye umiliki halali.

Lakini pia Kamishna uhakikishe unasitisha zoezi la ukataji na uuzaji wa viwanja lililokua linafanywa na Familia hii ya Kabeja pamoja na shughuli zozote za kibinadamu zilizokua zikiendelea hapa,” Amesema Mhe. Ndejembi.

Aidha amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kuacha kuvamia maeneo ambayo siyo yao na kujimilikisha pasipo kufuata utaratibu wa kisheria lakini pia akiwasihi pia wenye maeneo kutoyaacha kwa muda mrefu bila kuyaendeleza ili kuzuia kuibuka kwa migogoro ya ardhi isiyo na lazima.
 
View attachment 3316598

Sawa kabisa,na madalali nao wanawaingiza watu mikenge ili wapate Chao!
 
Hivi Wizara ya Ardhi kwa nini hadi karne hii kuna haya matatizo Tanzania

1. Ujenzi holela hata kwenye maeneo yaliyopimwa.

2. Hakuna uniformity kwenye ujenzi wa nyumba kulingana na maeneo, mathalani eneo moja unaweza ukakuta nyumba hii imeelekea mashariki na nyingine kaskazini.

3. Migogoro ya ardhi hadi kwa walio na hati.
 
Kisheria imekaaje hii, ikiwa siku huyu waziri hayupo madarakani au watendaji ndani ya wizara hawapo huyu bwana hawezi kuliamsha usumbufu ukaanza tena upya?
 
Hivi Wizara ya Ardhi kwa nini hadi karne hii kuna haya matatizo Tanzania

1. Ujenzi holela hata kwenye maeneo yaliyopimwa.

2. Hakuna uniformity kwenye ujenzi wa nyumba kulingana na maeneo, mathalani eneo moja unaweza ukakuta nyumba hii imeelekea mashariki na nyingine kaskazini.

3. Migogoro ya ardhi hadi kwa walio na hati.
hua wanajjibu hawa?
 
hua wanajjibu hawa?

Sikuwahi kujua kuwa kuna hii ID ya wizara, nimeona niulize kwa sababu kati ya vitu kama nchi tumevurunda ni ujenzi holela tena wa hovyo...
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Sikuwahi kujua kuwa kuna hii ID ya wizara, nimeona niulize kwa sababu kati ya vitu kama nchi tumevurunda ni ujenzi holela tena wa hovyo...
ni kweli mkuu -- mambo ni yaleyale ujenzi wa kihunzi -- kuingizana mkenge kwenye viwanja

lakini hawa jamaa huwa hawajibu yani kama hapa wao washamaliza tusubiri uzi wao mwengine

sasa sijui wanakua wamekuja kufanya nini jf
 
simple tu.sio mpaka msumbuane mahakamani.amekuja na vielelezo vyake apeweee
 
Back
Top Bottom