Waziri Ndejembi amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 7 wa Wizara ya Ardhi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
WAZIRI NDEJEMBI AMEMUELEKEZA KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI 7 WA WIZARA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi saba wa wizara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za makosa waliyofanya kwenye sekta ya Ardhi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam, wakati alipokutana na watumishi hao ambao wamekiri kuhusika na baadhi ya migogoro ya ardhi katika mkoa huo ambapo kupitia kikao hicho, Waziri wa Ardhi amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuihusisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kushughulikia suala hilo.

Baadhi ya changamoto katika sekta ya ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, zimebainika baada ya watumishi wanaotuhumiwa kukiri kuhusika moja kwa moja na tuhuma zinazowakabili kufuatia kupitiwa kwa majalada ambayo watumishi hao walikua wakiyafanyia kazi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Lucy Kabyemera pamoja na watendaji wengine wa wizara.

Your browser is not able to display this video.
 
Watajwe tuwajue kabisa.
 
takataka tupu including you! Takataka
 
Mbona makosa yao hujayaorodhesha sasa ?Weka taarifa kamili bana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…