Waziri Ndejembi azindua mkutano wa wadau wa mpango mpya wa uendelezaji Osterybay na Masaki

Waziri Ndejembi azindua mkutano wa wadau wa mpango mpya wa uendelezaji Osterybay na Masaki

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG-20250428-WA0052.jpg

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi April 28, 2025 amezindua mkutano wa kwanza wa wadau kwa ajili ya marejeo ya mpango wa uendelezaji upya wa eneo la Oysterbay na Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano huo, Mhe. Ndejembi ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wanapoendelea na mchakato huo wa utekelezaji kuhakikisha kila mdau anahusishwa kikamilifu katika kutoa maoni yake kwa uwazi, uhuru na kuzingatia maslahi mapana ya jamii.

Mhe. Ndejembi amesisitiz mpango mpya uzingatie mazingira ya sasa ya kijamii na kiuchumi, ikiwemo mabadiliko yaliyotokana na kuhamia kwa makao makuu ya nchi Dodoma.

“ Nisisitize pia kuhakikisha uendelezaji wa fukwe na mandhari ya asili ya eneo la mpango uzingatie kanuni za uendelevu, uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha kuhakikisha mpango huo unafungamanishwa na mpango kabambe uliopo lakini pia sekta binafsi ipewe nafasi stahiki lakini kwa kufuata miongozo ya maendeleo ya miji na kulinda haiba ya maeneo haya ya hadhi ya juu,” Amesisitiza Mhe. Ndejembi.

Mpango huu shirikishi umetayarishwa na Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri zote na umejengwa katika Dira ya kuwa na Jiji endelevu lenye ushindani kiuchumi linalotumia rasilimali zake kiufanisi na kuhifadhi mazingira.
 
Endelezeni vingunguti pale panatia aibu,ukiwa angani yaan unatua JNIA loh
 
Nawashauri achaneni na huko, komaeni na buguruni, kigogo, na Tandale.
 
Endelezeni vingunguti pale panatia aibu,ukiwa angani yaan unatua JNIA loh
Sheikh hakuna atayejali wanaangalia kwanza kwao ambapo ndio makazi yao yalipo huko kajamba nani pambaneni na hali zenu.
 
Back
Top Bottom