Waziri Ndejembi: Serikali kuanzisha chombo cha kuwasimamia madalali

Waziri Ndejembi: Serikali kuanzisha chombo cha kuwasimamia madalali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amesema ukosefu wa chombo cha kuwasimamia Madalali katika sekta ya ardhi umekuwa ukisababisha ongezeko la migogoro mingi katika sekta hiyo.

Ndejembi ameeleza hayo Ijumaa Mei 23, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Serikali imeona sasa wakati umefika wa kuweza kuanzisha chombo kitakachosimamia mawakala wanaofanya biashara au wanaodili na jambo lolote linalohusiana na umiliki ili wote wasajiliwe, watambuliwe, wafahamike na wafanyakazi sehemu gani," amesema.

 
Wewe uliyeposti huu ujinga huna tofauti na huyu aliyesema..
Serikali ina watu wajinga sana! Aliyeanza kusema kuwe na mamlaka ya kusimamia sekta ya milki ya nyumba ni waziri makamba..leo zaidi ya miaka 8 serikali inarudia kitu kile kile..mawaziri 4 wamepita hapo hakuna lolote lililofanyika, na huyu badala ya kutaja sababu zinazochelewesha kuanzisha hiyo mamlaka ya kusimamia milki ya nyumba..anarudia yale yale wenzake wanne waliopita walisema, km sio ujinga na kukosa akili ni nini..?
 
Jambo zuri. Real Estate agents wanatakiwa kuwa na mafunzo na leseni.
 
Aisee. Ndio maana ya uwepo JF. Umetoa wazo zuri.
 
Back
Top Bottom