Waziri Ndejembi: Tuwajengee Watanzania Makazi bora ya gharama nafuu

Waziri Ndejembi: Tuwajengee Watanzania Makazi bora ya gharama nafuu

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kutekeleza malengo yake ya msingi kwa kuwajengea watanzania wa kipato cha chini makazi bora na yenye gharama nafuu.


Mhe Ndejembi ameyasema hayo leo Agosti 07, 2024 wakati akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa NHC kwenye ziara yake ya kujitambulisha kwa watumishi wa shirika hilo baada ya kuteuliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Julai 21, 2024.

“Tusisahau kuwajengea watanzania maskini makazi bora na yenye gharama nafuu. Tuweke mipango madhubuti kuhakikisha tunatimiza azma hii. Shirika lazima liendelee na miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi hususani wale wa kipato cha chini.'

Soma Pia: Nyumba na makazi bora kwa raia yenye kuleta tija kwa maendeleo ya taifa letu

“ Ni lazima tuhakikishe hakuna wizi wala ubadhirifu wa fedha za umma hasa katika ununuzi wa ardhi. Ni muhimu kuzingatia uhalisia wa ardhi tunayoinunua,” amesema Mhe. Ndejembi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amelipongeza Shirika hilo kwa kuanzisha mpango wa Samia Housing Scheme ambao unalenga kujenga nyumba 5,000 ambapo awamu ya kwanza limeanza kujenga nyumba hizo katika jiji la Dar es Salaam na nyumba 560 nyingine zinatarajiwa kujengwa Dodoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah amemhakikishia Mhe. Waziri Ndejembi kwamba shirika hilo litaendelea kutekeleza malengo yake ya msingi ya kujenga nyumba zenye ubora na gharama nafuu kwa kuzingatia kipato cha kila mtanzania.
 
Ila hii definition ya bei nafuu huwa ni ngumu sana kuielewa.
utaona wanasema ni nei nafuu ila zinaanzia milion 30 .

Nashauri NHC wangalie aina ya technologia ya ujenzi wa Low cost housing.Wahandisi wetu wawe watafiti.Wanaweza Wakajifunze Rwanda inaenda vizuri kwa hili.Kuna hili shirika lina mradi huko kwa Kagame Skat Consulting Ltd. linashughulika na low cost housing
 
Mngejenga nyumba zenye thamani ya kipato cha Watanzania, yani chini ya Dollar mbili kwa siku
 
Unamaanisha Nyumba za mabati kama zile za pale Kenya? 😆😆...
Safe Simple or Complex residential structures but ziwe cheap kwa raiaa Lengo lao lisiwe kupata faida, lengo iwe ni kutoa huduma kwa Wananchi!
 
Safe Simple or Complex residential structures but ziwe cheap kwa raiaa Lengo lao lisiwe kupata faida, lengo iwe ni kutoa huduma kwa Wananchi!
Hawawezi hao... maneno tu.
 
NHC lost the Plot way back..., Hata sijui tena Their Vision, Mission or Objective..., wamechukua assets na ardhi ambayo mission yake ilikuwa affordable housing na kujibadilisha na kugeuka kuwa a for profit institution competing with private real estates, building houses which majority can not afford...
 
Utasikia satellite apartment yaani chumba kimoja na sebule, choo na jko milioni 30. Kwa gharama hizo sidhani Mtanzania wa kipato Cha kati atashawishika achilia mbali wa kipato Cha chini.
 
Back
Top Bottom