BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Ndumbaro amesema mapungufu mengine ni sheria kutomwangalia mwathirika ambaye anaweza kuwa amedhulumiwa mali zake lakini wakati wa majadiliano DPP anamalizana na Mshtakiwa huku fedha zinazolipwa kwa Plea Bargain zikibaki Serikalini.
Akizungumza kupitia Power Breakfast ya CloudsFM, Waziri Ndumbaro amesema kutokana hilo, Serikali imeandaa mabadiliko ya Sheria yatakayoruhusu Mahakimu na Majaji kutoa hukumu zenye fidia kwa Walalamikaji.
================