Waziri Ndumbaro Apongeza Ubora wa Jengo la Wizara

Waziri Ndumbaro Apongeza Ubora wa Jengo la Wizara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI NDUMBARO APONGEZA UBORA WA JENGO LA WIZARA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepongeza ubora wa jengo jipya la Wizara hiyo linalojengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba na kumtaka mkandarasi akamilishe kazi zilizobaki ifikapo Septemba, 2024.

Mhe. Ndumbaro ametoa pongezi hizo Juni 5, 2024 baada ya kukagua hatua za ujenzi huo, ambao tayari umefikia asilimia 86.

"Nimemsisitiza mkandarasi aongeze kasi ya ujenzi na ameahidi kukamilisha Septemba 30, 2024 ili watumishi waanze kulitumia.

Jengo hilo linajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

GPUenKoW4AAqDDB.jpg
GPUenAAWgAAo1XA.jpg
GPUenSUWwAAnhV7.jpg
GPUenSaW0AAuYoe.jpg
 
Back
Top Bottom