Waziri Ndumbaro azindua kitabu cha kuboresha mazingira ya kazi, asisitiza wazawa kuandika zaidi

Waziri Ndumbaro azindua kitabu cha kuboresha mazingira ya kazi, asisitiza wazawa kuandika zaidi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ndumbaro.jpg


Waziri wa Katiba na Sheria, DR. Damas Ndumbaro ameshiriki katika uzinduzi wa Kitabu cha COMPREHENSIVE ISSUES OF EMPLOYMENT AND LABOUR RELATION AND LABOUR LAW; Practice for Modern Business in Tanzania.

Kitabu hicho kinahusu masuala ya ajira na masuala ya uhusiano kazini kikiwa na kurasa zaidi ya 800.

Akizungumzia kitabu hicho katika uzinduzi uliofanyika Januari 25, 2023 jijini Dar es Salaam, Waziri Ndumbaro ametoa pongezi kwa Wakili Ally Kileo na MDM Law Group na kuongeza kuwa Taaluma ya sheria tangu zamani imejiweka katika nafasi ya kipekee kuwa ili uwe mwanasheria unatakiwa kutunza na kudumisha tabia ya kusoma vitabu vya sheria na fasihi za taaluma nyinginezo.

Ameongeza kuwa kitabu hicho kimekuja muda sahihi katika wakati ambapo taaluma ya Sheria na nyinginezo zinahitaji nyenzo/fasihi zinazoweza kuwaongoza wanafunzi na wataalamu.

Amesema kuwa huo ni mwendelezo mzuri wa machapisho ya waandishi wa ndani na amekuwa akisisitiza Watanzania kuwa na tabia ya kuandika.

Aidha, Mwandishi wa kitabu hicho Wakili Ally M.Kileo amebainisha kuwa ametumia miaka mitano kuandaa kitabu hicho na kuwa lengo ni kuelimisha waajiri, wawekezaji, waajiriwa, wajasiriamali, mawakili, wanasheria, vyama vya wafanyakazi, watafiti, wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu.

Ameongeza kuwa kitabu hicho kinatarajiwa kuziba mapengo ya mianya iliyopo kwenye tasnia husika hasa kwa Afrika na zaidi ikiwa ni Nchini Tanzania.

Wakili Kileo ameongeza kuwa kitabu kinatarajiwa kusambazwa kwenye maduka mbalimbali Nchini pia kitapatikana kwa njia ya mtandao.
 
Hongera zao sana waandishi. Kuandika kitabu ni kazi ngumu mno inayohitaji umakini mkubwa na kujitoa...
 
Back
Top Bottom