Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Akizungumza katika kongamano la huduma ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki kwa wananchi linalofanyika mkoani Arusha jana Alhamisi Agosti 17, Dk Ndumbaro amehoji kutokamatwa kwa Prof. Anna Tibaijuka na wengine ambao wamekosoa mkataba wa bandari. Ndumbaro amesema kukatwa kwa Dkt. Slaa na wengine hakuhusiani na mkataba wa bandari
Ndumbaro amesema kuna watu wanataka kutumia hekima za kimagharibi Tanzania ilhali hapa kumtukana Rais ni kosa.
======
Dkt. Ndumbaro: Nchi zilizoendelea Mtu kuvaa chupi na sidiria wakati wa Summer hiyo ni hekima, sasa Tanzania kufanya hivyo ni hekima?, kila Mtu atakushangaa, sasa kosa letu tunataka kutumia hekima ya kimagharibi kuileta hapa, sisi kwetu kumtukana Rais sio hekima, uchochezi haiwezi kuwa hekima, kuigawa Nchi kwa itikadi mbalimbali haiwezi kuwa umoja
Uhuru wa maoni sio haki pekee ya Binadamu kuna haki nyingine ambazo wakati unatekeleza uhuru wako wa maoni lazima uzingatie hizo nyingine, kuna tofauti kati ya kauli za kukosoa na kauli zinazovunja haki za wengine, kutukana Viongozi na kauli zako zikileta makosa ya jinai uhuru wako unaishia hapo na tutaanza kukushughulikia
Kukamatwa kwa Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mdude hakuhusiani na mkataba wa Bandari, kuna Watu walikosoa sana mkataba ule na mmoja ni Prof.Tibaijuka hivi amekamatwa?, na hata juzi alihojiwa na Vyombo vya Habari vya Kimataifa akaendelea kukosoa, ila amekosoa bila kukiuka sheria yoyote
TLS walitoa waraka wao kukosoa, Sungusia ndiye anaongoza TLS na yupo hapa, Sungusia wewe ulikamatwa?, waliofungua kesi ya Bandari kule Mbeya ambao wameiburuza Serikali Mahakamani hakuna aliyekamatwa