Waziri Ndumbaro: Uwanja wa mpira Arusha utakamilika kwa wakati kwa michuano ya AFCON 2027

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amesisitiza kuwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kuwa tayari kwa michuano ya AFCON 2027.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya uwanja huo leo Agosti 29, 2024 Dkt. Ndumbaro amewahakikishia Watanzania kuwa ujenzi wa uwanja huo utakamilika kwa wakati kutokana na kasi na uwezo wa mkandarasi anayetekeleza ujenzi huo.

Soma Pia: Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Amewataka wananchi wa Arusha na maeneo mengine waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali ili maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza, kuendeleza na kukuza fursa za ajira kwa Watanzania kupitia sekta ya michezo yaweze kutimia kupitia mradi huo.
 
Ujenzi wa uwanja mpya unaendelea vizuri ila ukarabati wa Mkapa, aaah!

Jina la uwanja ni refu sana. Utasikia wanaongeza na "Muheshimiwa Dr. Mama....."
 
Back
Top Bottom