Waziri Ofisi ya Rais ‘Kazi Maalum’ ana majukumu gani?

Waziri Ofisi ya Rais ‘Kazi Maalum’ ana majukumu gani?

Waziri wa TISS nadhani,kwa sababu alikuwepo Siyovelwa,Munanka,walikuwa wanafanya kazi ya TISS,wote walikuwa wanaitwa Waziri( asiye na) kazi maalum. Minister without portfolio.
 
Huyu kazi yake kukoleza moto kwa ajili ya chetezo wakati wenzake wakiwa na paroko ndani ya muda wanafukizia ubani. Ni mtu muhimu sana. 😆😆😆😆😆😆😆😆
 
Sawa na kamati ya ufundi kwenye timu ya mpira.
Ulishawahi kujiuliza wana kazi ya ufundi gani wakati mafundi wa mpira wako uwanjani?
 
Huyu mkuchika waziri wa hiyo ofisi ni mgonjwa muda mrefu nakumbuka hata wakati mawaziri wenzake wanaapishwa yeye hakula kiapo alikuwa amelazwa.
Mimi sikubaliani na hiki cheo ni matumizi mabaya ya raslimali za nchi.
Kazi maalumi zifanywe na TISS tu kupitia wizara ya utumishi na utawala bora
 
Kuwepo kwake kwenye mfumo kwa muda mrefu kunamuweka kwa sabab wanazozijua wenyewe wa huko mfumoni
 
Back
Top Bottom