Waziri Patrobas Katambi: Gerezani siyo sehemu ya adhabu tu, ni sehemu ya uzalishaji
Serikali imeweka wazi kuwa Magereza mbalimbali nchini sio Sehemu ya Mateso huku ukiwepo ushahidi wa Maendeleo kwa Wafungwa kuhitimu Masomo ya ngazi mbalimbali na Mafunzo wakiwa ndani ya kifungo ikiwemo Wafungwa 209 waliohitimu Masomo ya Ujasiriamali katika Chuo cha Uhasibu Arusha na wafungwa 201 waliopata vyeti kutoka Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA).
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema hayo alipokuwa Msalato jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea Jeshi hilo ambapo aliongozana na Naibu Waziri, Ayoub Mohamed Mahmoud.