Waziri Patrobas Katambi: Kitambulisho cha NIDA sio taarifa binafsi. Ni Public na ndio maana mnasheherekea Birthday

Waziri Patrobas Katambi: Kitambulisho cha NIDA sio taarifa binafsi. Ni Public na ndio maana mnasheherekea Birthday

Personal data protection act 2022 ( sheria ya kulinda taarifa binafsi za mtu) ndio inatueleza nida nitaarifa binfsi na sio public waziri amepotoka
 
Kisheria na kiusalama, namba ya NIDA au maelezo yaliyopo kwenye kitambulisho hicho yanaangukia kikamilifu kwenye kundi la Taarifa Binafsi (Personal Data) kwa sababu yanamtambulisha mtu moja kwa moja.
Hapa kuna sababu kuu tatu kwa nini kitambulisho cha NIDA ni taarifa binafsi:
Hubeba Utambulisho wa Kipekee: Namba ya NIDA (NIN) ni ya kwako peke yako nchi nzima. Hakuna mtu mwingine mwenye namba kama hiyo.
Inajumuisha Taarifa Nyeti: Kitambulisho hicho kina jina lako kamili, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, na picha yako. Pia, kimeunganishwa na alama zako za vidole (biometrics) na saini yako.
Ulinzi wa Kisheria: Chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 nchini Tanzania, taarifa zote zinazomfanya mtu atambulike (ikiwemo namba za vitambulisho vya kiserikali) zinalindwa kisheria. Ni kosa kuziweka wazi, kuzisambaza, au kuzitumia bila ridhaa ya mwenye nazo au bila kufuata taratibu za kisheria.
 
Hivi PDPC anaifahamu huyu? Tume ya Kulinda Taarifa binafsi?
 
Katambi amepuyanga. Ukweli ni huu hapa:- NIDA ni component ya taarifa binafsi chini ya sheria ya mwaka 2022. Lakini kutoa NIDA unapoingia guest house siyo kuvunja sheria hiyo.

1. Agizo hili halilengi kuingilia faragha, bali ni hatua ya kiusalama (National Security) kufuatilia wahalifu au wageni wanaoingia nyumba za kulala wageni.

2. Kama mteja hana kadi ya NIDA, anaweza kutumia nyaraka nyingine rasmi kama leseni ya udereva, pasipoti, cheti cha kuzaliwa, au kitambulisho cha mpiga kura

3. Ili wasikiuke sheria, wamiliki wa gesti wanatakiwa kuwa wamesajiliwa na Commission ya Personal Data Peotection kama "Wakusanyaji wa Taarifa" na wana wajibu wa kulinda daftari hizo zisomwe na watu wasiohusika.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema kutoa Kitambulisho cha Taifa (NIDA) unapotembelea nyumba ya kulala wageni hakumaanishi kuanika taarifa binafsi, kwani kitambulisho hicho si taarifa binafsi.

Soma Pia: Waziri Katambi: Wamiliki wa Hoteli, AirBnB, Guest Houses na Lodge nchini wasajili wageni wote kwa kutumia kitambulisho cha NIDA

Akizungumza Juni 29, 2026, jijini Dodoma alipokuwa akizungumza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Katambi amesema taarifa zilizopo kwenye Kitambulisho cha Taifa si za siri, ndiyo maana hutolewa pale zinapohitajika katika taasisi au maeneo mbalimbali, hata katika mazingira ya wazi

"Kitambulisho cha taifa sio taarifa binafsi. Taarifa binafsi.. kitambulisho cha taifa ni public na ndio maana umesajilia namba ya simu eh... NIDA yako umejisajili, umeionyesha popote, umeipiga fotokopi, umeambatanisha kwenye mikataba ya kuuziana ardhi na nini, hio sio taarifa binafsi. Particular za mtu za yeye ni nani, eh anaishi wapi, ana umri gani, hizo sio taarifa binafsi. Ni public kwa sababu kila mahali lazima mtu utaulizwa hivyo, na ndio maana mnafanya na birthday."


 
Wanataka watanzania waanze kulala nje kama wanyamapori..... 🤣 Hao ndio mlio wachagua wawaongoze.....
 
Kwa hiyo nikienda ofisi za NIDA kuhitaji taarifa za mtu mwingine napewa sababu ni public?

Au kwake hiyo ID anaona ina tarehe ya kuzaliwa pekee?

Huyu atakuwa amechangia anguko la SMG ya Dialo,alikuwa muajiriwa pale!!
 
WATU WAJINGA WAJINGA WANAPOBAHATIKA KUPATA UONGOZI....HASARA YA KWANZA TUNACHOCHEA HALAIKI YA WATU WAJINGA WAJINGA THEN TUNAIDHALILISHA NAFASI YA UONGOZI ALIYOKUWA NAYO!!

Kuna viongozi unawasikiliza unabakia na maswali kuwa sio tu kuwa kiongozi huyu aliwezaje kufaulu hata darasa la saba
 
Mtu anatoa maelekezo ya kijinga, badala ya kuchutama na ku reflect, anazidi kuongea ujinga kusafisha ujinga wa Awali
 
Back
Top Bottom