JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Taarifa kutoka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa, mnamo tarehe 8, Mei 2024, Waziri aliunda Kamati Maalum ya uchunguzi yenye jukumu la kuchunguza malalamiko hayo na kubaini ukweli wake.
Baada ya kamati kukamilisha uchunguzi iliwasilisha taarifa ya yaliyobainika kulingana na tuhuma zilizowasilishwa. Kamati ilijidhihirisha pasi na shaka kuwa uongozi ulikuwa na mapungufu ya kiutendaji.
Mapungufu yaliyobainika ni matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Sheria za nchi, Katiba ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania ya mwaka 2018 pamoja na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na usimamizi wa rasilimali za kamisheni.
Matumizi mabaya ya fedha kinyume na Sheria za nchi, Katiba ya Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania 2018 pamoja na kanuni za uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za kamisheni.
Kufuatia mapungufu hayo, Mheshimiwa Waziri ameelekeza hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya viongozi walioondolewa madarakani, ili kuweka fundisho kwa viongozi wengine wa vyama na mashirikisho na michezo nchini.
============================
Awali walivyosimamishwa
Awali walivyosimamishwa