Waziri Riziki Pembe: Lengo la Kampeni ya MTOTO NI MBONI YANGU ni kutokomeza ukatili na unyanyasaji Wanawake na Watoto

Waziri Riziki Pembe: Lengo la Kampeni ya MTOTO NI MBONI YANGU ni kutokomeza ukatili na unyanyasaji Wanawake na Watoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
“Tumezindua rasmi kampeni hii ya Mtoto ni Mboni yangu ambayo itafanyika mwezi Novemba katika Mikoa yote mitano ya Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba na lengo la Kampeni hii ni kutokomeza matukio yote ya ukatili na unyanyasaji kwa wakina mama na watoto kwani hilo ndio janga kubwa linaloharibu familia zetu na Zanzibar bila Unyanyasaji inawezekana” Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe.

WhatsApp Image 2024-10-26 at 12.03.39_bc23707c.jpg


Hotuba Ya Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto, Riziki Pembe Juma Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Kutoa Taarifa Ya Kampeni Ya Kitaifa Yenye Jina La “MTOTO MBONI YANGU”, 25/10/2024 Katika Ukumbi Wa Wizara Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto - Kinazini Zanzibar

Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema ya uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana siku ya leo kwa ajili ya kutoa taarifa ya KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA MTOTO MBONI YANGU.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto Ajira” kutoka Dar es Salaam imeandaa kampeni ya kitaifa yenye jina la MTOTO MBONI YANGU, ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Zanzibar.

Lengo kuu la kampeni hii ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuizunguka nchi nzima ya na kuielimisha, kuiasa na kuzungumza na Wazanzibari wote wakiwemo wanafunzi, viongozi wa dini, vijana, watoto na jamii kwa ujumla juu ya kupinga vitendo vyote vya ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto, Vijana, Wanawake na Wazee. Ili kwa pamoja tuweze kuwalinda watoto na vijana wetu dhidi ya mmong’onyoko wa maadili.

Kampeni ya MTOTO MBONI YANGU imeanza Oktoba 23, 2024 na itaendelea hadi tarehe 30 Disemba 2024, kwa ufupi ni kampeni ya miezi miwili.
WhatsApp Image 2024-10-26 at 12.03.37_ae7be021.jpg

WhatsApp Image 2024-10-26 at 12.03.33_d2db5783.jpg
Aidha, Kampeni ya MTOTO MBONI YANGU itazinduliwa pia kwa mbio za Marathon siku ya Jumamosi ya tarehe 23 Novemba 2024 katika viwanja vya Mao Tse Tung na kufungwa katika visiwa vya Pemba. Ni imani yangu kwamba jamii itaunga mkono juhudi hizi.

Kampeni hii imekuja ikiwa na azma ya kuunga mkono juhudi za mhe Rais wetu wa Zanzibar na M\kiti wa Baraza la Mapinduzi Dr HUSSEIN ALI MWINYI na Serikali ya awamu ya nane ambapo tunaziona juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali yetu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu na kupambana na vitendo vyote viovu vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia.

Kupitia Kampeni hii, Wizara inategemea kukusanya kiasi cha Tsh 650,000,000/= ambazo zitatumika katika utekelezaji wa kampeni hiyo. Hivyo, tunaiomba jamii, kuitikia wito huu kwa kuchangia fedha ili zoezi hili liweze kufanikiwa kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
Marathon yetu inatarajiwa kujumuisha takriban washiriki 20,000, kutoka Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara wakiwemo watoto, vijana, wanawake, watu wazima kwa jinsia zote na hali zote bila kumuacha mtu nyuma (wakiwemo na watu wenye ulemavu).

Washiriki wote wa Marathon watapewa medali baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 (nusu marathon), kilomita 10, na kilomita 5, huku washindi watano wa

Mwanzo watapewa zawadi za fedha taslimu.

Ndugu waandishi wa habari,
MTOTO MBONI YANGU MARATHON ni Marathon ya kwanza kufanyika ndani ya Zanzibar. Tunaomba wananchi wote na wadau wote kujitokeza kuchangia kampeni hii. Tutoe wito kwenu pia ndugu wana habari kuwa wa kwanza kujitokeza kuchangia kwani shilingi yako moja ndio mwanzo wa hesabu. Hii ni nafasi ya kipekee kwa kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ya Mapinduzi Zanzibar ya awamu ya nane katika kulinda vizazi vyetu viwe vyenye maadili mema kwa maendeleo ya taifa letu.
WhatsApp Image 2024-10-26 at 12.03.31_268b462b.jpg
Gharama ya kujisajili kwa mtu mmoja mmoja ni Tsh 30,000 ambapo mshiriki atapata Tshirt na namba yake.

Pia kwa mara ya kwanza tumeleta package kwa makampuni na Taasisi mbalimbali kuchangamkia package hizi ambazo ni :

Package ya milioni 1,000,000 ambapo kampuni au taasisi itaweza kupata T-shirt 10 za marathon, logo zao kuonekana kwenye red capert, kukaa sehemu maalumu siku ya marathon pamoja na kutunukiwa cheti maalumu.

Package ya 500,000 ambapo kampuni au taasisi itaweza kupata T-shirt 5 za marathon, logo zao kuonekana kwenye red capert, kukaa sehemu maalumu siku ya marathon na kutunukiwa cheti maalumu.
  • Kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kulitokomeza janga hili ndani ya nchi na Taifa letu ili kuwa na kizazi chenye maadili mema, kinacho weza kuchangia mustakabal bora wa taifa letu.
  • Zanzibar bila ya udhalilishaji inawezekana sana endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.
Pia soma:
~ Matukio ya Ukatili wa Kijinsia yaripotiwa kuongezeka Visiwani Zanzibar
~ Mkuu wa Wilaya ya Mafia: Watoto 15 wamelawitiwa na Ustadhi wa Madrasa Kisiwani Mafia
~ Zanzibar: Nani anamlinda Ustadhi wa Madrasa anayedaiwa kumbaka na kumpa ujauzito binti wa Miaka 16?
~ Uhalifu 2023: Zanzibar yaongoza ubakaji, Arusha yaongoza ulawiti
~ Zanzibar: Afungwa miaka 70 jela kwa kubaka, kulawiti na kutorosha msichana
 
Back
Top Bottom