TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

radio tanzania wametangaza,wamesema ni kweli kafariki,ukitaka kusikiliza online ingia radio maria station,kwani wanaingiliana vipindi na radio tanzania
 
Bbc swahili wamesema kweli katutoka mhesh Mbatia.R.I.P
 
Mhe. Mbatia amepoteza maisha yake pamoja na dereva wake.

Kwa upande wa lorry, wamepoteza maisha watu wawilli na wengine wawili wapo hospitali. Hii nikutokana na habari ya Channel 10
 
Nyumbani kwa Marehemu Uganda Avenue, Oystebay
 
nasikiliza bbc swahili LIVE naona hawajui bado au ndio wanasubiri waambiwe na IKULU.

mungu amlaze mahali pema.


Mkuu nadhani utakuwa umenote wameisema mwisho, nilikuwa nimejipumzisha kuamka nikaingia kwenye website kuwasikiliza, ndo wakatangaza kama breaking news, kukimbilia hapa JF nakuta habari 'imeshachakaa'

Mungu ailaze roho ya marehemu na wengineo wote mahali pema peponi, it is digustng kupoteza viongozi wetu that way, na mwaka huu unaonekana mbaya kweli ......
 
Oooh God!!! RIP mama Salome Mbatia na poleni wafiwa wote
 
mie nashangaa watu wengi wanaona upande mmoja wa shillingi wakati tumeambiwa roho nne zimepotea pale..jamani Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi na kuzifariji familia zao na kuwapa nafuu ya haraka majeruhi...
nasi tujiandae kwa safari zetu zikifika tuwe tayari
 
Inasikitisha na kuhuzunisha lakini ndiyo maisha. kuna kuja na kuondoka kwa staili mbali mbali. Mungu aziweke Roho za Marehemu mahali pema peponi na aendelee kuwafariji Familia zao.
 
na kuhusu hizi ajali wajimini za viongozi wetu hawa ndo tusem mwaka wa shetwani ama??ajali zimezidi wajimini keleuwiii
 
Oh dear...Poleni familia za wafiwa.

Maskini Mama wa watu alikuwa na roho ya upendo sana. Lakini watu aliofanya nao kazi walikuwa wakimwogopa kama ukoma.

God bless the departed souls. Amen!
 
Labda sahihisho kidogo tu, tuseme roho ZA marehemu..


swadakta, mwenyezi Mungu azilaze roho za Marehemu wote peponi. Mniwie radhi. Na kichwa cha habari kibadilishwe kidogo.. "Waziri Mbatia na wengine wafa Ajalini"... or something ..
 
Mwenyezi Mungu awahurumie Marehemu madhambi yao, na awapumzishe pema. Majeruhi nao wapate nafuu haraka. Poleni sana wafiwa wote.
 
Kisura Iam so sorry to write this: "uliyoyaandika hapo juu ni UNAFIKI WA HALI YAJUU! eti alikuwa na roho ya upendo lakini alikuwa anaogopwa" Kauli kama hizo ni mbaya saana. Kwa nini watu tunapenda kuwa wanafiki? we sema pole thats enough kila mtu atakuelewa. WATANZANIA TUMEZIDI KWA UNAFIKI, MPAKA LINI?.

Again Iam sory kukujulisha haya niliyoyaandika. But Iwas unconfortable na nimeona nikwambie tuu.
 
Habari zaidi kutoka RTD saa mbili ni kuwa Makamba amethibitisha habari hizo.....na hadi sasa wanajitahidi kupeleka miili ya marahemu hospitali ya Kibena kisha Dar es Salaam
 
WanaJF

The bad part is that. Mpaka sasa bado hawajaweza kutoa miili ya marehemu waliokuwa katika gari ya Mama Mbatia. Hii nikutokana Taarifa ya Habari ya TVT ya saa mbili!
 
hivi marehemu ana uhusiano wowote na mbatia wa nccr mageuzi

Ndiyo walikuwa wana uhusiano. Ni mashemeji. Salome Mbatia ni mke wa Dr Joseph Mbatia (Medical Dr), ambaye ni kaka wa James Mbatia wa NCCR. Pamoja na kuwa vyama pinzani ki-siasa, hawa (Salome na James) walikuwa very close in the family circles.

Mungu awarehemu wafiwa na majeruhi, na awape subira ndugu na jamaa.
 
Back
Top Bottom