Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Dunia inazunguka kwa kasi sana, hii barabara inazibwa viraka sasahivi kule swaswa
 
Hawa huwa hawamkimbizi kuku, akija mgeni, kuku ananyooshewa kidole anakuja mwenyewe kuchinjwa.
 
Just imagine, yaani mkandarasi anasemwa na waziri kwa kuchelewesha kazi hadi mkandarasi anazimia kabisa, huu si uuaji jamani? Na ni udhalilishaji pia, hayo ni maoni yangu. Angalia video hapo mwishoni kabisa.
---


Mkurugenzi wa kampuni ya SCOL Building Contractors Limited Vicent Massawe, ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara

======

Dodoma. Mkurugenzi wa kampuni ya Scol Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara.

Kutokana na kuchelewa huko mkandarasi huyo amekatwa Sh80 milioni na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

Licha ya kujitetea kuwa wamejenga katika miradi mingi nchini ikiwemo katika jimbo la Kisarawe ambalo mbunge wake ni waziri huyo wa Tamisemi, waziri huyo alikataa na kubainisha kuwa uwezo wa kampuni hiyo ni mdogo.

Baada ya hoja hiyo kupanguliwa na Jafo, mkurugenzi huyo alijitetea kuwa anakwamishwa na upatikanaji wa malighafi.

“Si watu wengi wanaweza kutumia hii nyenzo, hili jiwe hili linatoka Lugoba, Sisi tunataka tufanye kazi nzuri,” alijitetea mkurugenzi huyo.

“Umeshatembelea kazi za wenzako ukafanya ulinganisho ,” amehoji Jafo na huku mkurugenzi huyo akikosa jibu.

Hali hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kusema inawezekana kuna kinachomfanya kuchelewesha kazi, ndio maana anashindwa kusema ukweli.

“Katika sehemu ambayo sina shaka na mkurugenzi wangu, mhandisi wa Mkoa wa Dodoma wala mkuu wangu wa Mkoa ni eneo hili la usimamizi wa miradi kwa sababu miradi inaenda vizuri sana,” amesema Jafo.

Jafo amesema katika mradi huo changamoto ipo kwa mkandarasi, akibainisha kuwa Dodoma wamejenga barabara nyingi zimekamilika katika muda mfupi.

“Injinia kuna miradi mingine mmempatia hapa Dodoma,” amehoji Jafo na kujibiwa kuwa hakuna miradi mingine aliyopewa.

Alitoa agizo kwa viongozi wa Dodoma kutompatia mradi mwingine mkandarasi huyo huku akitilia shaka kasi yake ndogo na ubora wa barabara.

Jafo aliagiza mkandarasi huyo kuendelea kukatwa fedha hadi kazi itakapokamilika, kwamba ujenzi wa barabara hiyo unatakiwa kukamilika Desemba 30, 2019.

“Hizo blablaa zako za kokoto zinatoka mbali na nini sitaki kuzisikia, wenzako wote wanatengeneza barabara wanatoa wapi. Labda huna mtaji. Wakazi wa hapa wameteseka sana na madimbwi ndio maana tukasema tuunganishe hii barabara,” amesema Jafo.

Waziri huyo amesema ikiwa mradi huo hautakamilika Desemba 30 atawapiga marufuku wataalam wake wote kumpa kazi nchini.

“Wewe unakuja hapa ndio injinia ama mkurugenzi mbona sikuelewi. Ikifika tarehe 30 kazi hii isipokamilika hamtapata kazi yoyote nchini,” amesema Jafo na ghafla mkurugenzi huyo akaishiwa nguvu na kuanguka na Jafo kumtaka asimame na kusisitiza kuhusu Serikali kutotaka kufanya kazi na Mkandarasi mbabaishaji.

Chanzo: Mwananchi

Unapochukua contract lazima utathmi uwezo wako.Haya amejitakia.Unatoa visingizio wakati umeshapewa contract,alitakiwa kuona vitu ambavyo vingen-mkwamisha mapema.Uchu wa pesa tu.
 
Arusha wamekusanya billon 30 mapato ya ndani 2023-24 mpaka mwezi jana wametumia billioni 7, zimebaki billion 23.

Kwa kanuni za serikali ikifika muda wa budget kuu wilaya na mikoa ambazo wamebakiza mapato yao ya ndani wanapeleka hazina.

Wakati huo huo wenyeji wanashida kibao na hizo hela zingewasaidia miradi ya jamii yenye tija au kuboresha mazingira ya jiji.

Bado kuna hela za miradi walizopewa na serikali kuu kiasi kikubwa awajatumia kwa kazi zilizopangiwa; maana yake nini budget ijayo mgao wao kutoka serikali kuu unaweza pungua.

Wanaopoteza ni wana Arusha na serikali inaonekana aifanyi kitu, hayo yamebainishwa na Makonda muda mchache aliokaa hapo.

Uzembe ni shida huko mikoani, huko ni Arusha tu hatujui mikoa mingine wamebakiza kiasi.

Moja ya mistake kubwa aliyofanya ‘bi-tozo’ katika uraisi wake ilikuwa kumtoa Jaffo TAMISEMI sio kwa hakuna hela huko watu wanakaa nazo tu hawafanyii kitu wanatafuta namna ya kuzitafuna kwanza.

Tanzania ukiwa mchapa kazi kwa faida ya wananchi upendwi, nchi inapenda watu wavivu na wazembe wasiowajibika.
 
Back
Top Bottom