KERO Waziri Shemdoe alisema Mfumo wa PEPMIS usiwe kikwazo cha kutopanda daraja Watumishi, Wilaya ya Chemba tunateseka

KERO Waziri Shemdoe alisema Mfumo wa PEPMIS usiwe kikwazo cha kutopanda daraja Watumishi, Wilaya ya Chemba tunateseka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu kutoka Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma, tunacheleweshwa kupandishwa madaraja, tulitakiwa kupanda madaraja kuanzia Mei 2026, lakini hadi sasa hatujapandishwa wala kupewa maelezo ya wazi kuhusu sababu ya kuchelewa.

Tuliposubiri kupata majibu, baadhi yetu tuliwasiliana na Maafisa Utumishi, lakini tunaelezwa kuwa alama za PEPMIS hazitoshi, hivyo mtumishi hawezi kupandishwa daraja.

Hali hii inatuchanganya kwa sababu tulielezwa na Waziri Shemdoe kuwa mfumo wa PEPMIS haupaswi kuwa kikwazo cha mtumishi anayestahili kupanda daraja. Pia, hatujapatiwa elimu ya kutosha kuhusu mfumo huo na vigezo vinavyotumika kumpandisha au kutompandisha mtumishi.

Kinachotukatisha tamaa zaidi ni kukosa majibu ya wazi. Tunaomba mamlaka za Mkoa wa Dodoma na Halmashauri ya Chemba kutoa ufafanuzi kuhusu kinachoendelea, kwa sababu kucheleweshwa kwa madaraja kunaathiri maslahi na morali ya watumishi.
 
Kama uliambiwa alama za PEPMIS hazitoshi huo ndio ukweli sasa.
 
Na hilo liDED lenu lilivyo senge na halijui lolote sidhani kama litawasaidia. Linakazi ya kujisifu na kutisha watu tu kuwa unajua mimi ni nani?

Pumbavu kabisa na mamacho yake mekundu.
 
Back
Top Bottom