JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri Silaa ameagiza kutafutwa mtu mwingine mmoja anayefahamika kwa jina la Nida ili aweze kueleza jinsi alivyozibeba milioni 80 ambazo ni pesa za mauzo ya nyumba ya Li Shi Cai.
Waziri Silaa ametoa maagizo hayo mapema leo Aprili 18, 2024 alipotembelea eneo hilo lililopo katika mtaa wa Mwanjelwa jijini Mbeya ili kusikiliza na kutatua mgogoro huo.
Watu hao walichukua hatua ya kuuza eneo hilo baada ya kudhani Li Shi Cai amekufa na ugonjwa wa Corona hivyo eneo hilo kukosa mmiliki, wakati mtu alikuwa hai na hakuonekana kutokana na majukumu yake.