Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Polisi na mjitambi wapi na wapi!

Kutwa kubugia manyama, masukari, majwisi na matakataka ya kila aina!

Michemsho, mapombe, rosti, nguruwe, soda, machips..... baada ya mwaka tumbo kama litufe! Ooohh nimerogwa sikuwa hivi!

Kuzaa huzai, unajaza tu nafasi duniani. Ulafi na kukosa nidhamu ya chakula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakula sana mazagazaga mzee na kwa kitambi chako najua huwezi piga zaidi ya 2 kwa usiku mmoja.Pole boss.
Waafrika tuna asili ya unene...aache ujinga. Mimi nilipokuwa chini ya miaka 30 nilikuwa nawacheka sana watu wenye vitambi...nilikuwa nawaita manyama uzembe.

Ila sasa kitambi changu karibia kinagusa chini, GYM zote nimemaliza hadi yale madawa ya Forever Living yanaitwa C9.

Kama hayajakukuta shukuru Mungu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisi na mjitambi wapi na wapi!

Kutwa kubugia manyama, masukari, majwisi na matakataka ya kila aina!

Michemsho, mapombe, rosti, nguruwe, soda, machips..... baada ya mwaka tumbo kama litufe! Ooohh nimerogwa sikuwa hivi!

Kuzaa huzai, unajaza tu nafasi duniani. Ulafi na kukosa nidhamu ya chakula.

Sent using Jamii Forums mobile app
Teh teh teh...acha unyanyapaa mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu mavitambi mengine ni shidaa kwa wengine iwe kwenye vyombo vya usafiri wa umma, hospitalini hata wakifa kubeba maiti zao ni mziki mwingine.

Punguzeni kula na fanyeni mazoezi ya kina na pia mtembee hata kwa mguu siku mojamoja.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geogre Simbachawene, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, kuwaondoa askari wote wa Usalama Barabarani wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine kwani wamekosa sifa

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Kongamano ya Usalama Barabarani lililofanyika mjini Dodoma."Wapo Trafiki wanastahili kuondolewa kwa kukosa sifa ya kuwa trafiki!! Kwa mfano wa Trafiki wa Gairo wana vitambi! askari anakuwaje na kitambi?"- amesema Simbachawene na kuongeza kuwa;

"Wapo askari wa usalama barabarani ambao wamegeuza 'crown', sare nyeupe na kofia kudai rushwa kutoka kwa bodaboda, malori na kirikuu!! naelekeza trafiki kufanya kazi kwa weledi! tuache kusimamia sheria kwa mazoea!”

Amesema kuwa ajali zimekuwa zikigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi, kupoteza nguvu kazi ya taifa "Ajali hizi zimekuwa zikiigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

"Serikali kupitia wizara yangu ipo katika mchakato wa kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani 1973, ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa" amesema Simbachawene

Amesema kuwa wapo madereva wanaendesha magari wakiwa wamelewa; wapo watembea kwa miguu wanavuka barabara wakiwa wamelewa; wapo madereva wanaendesha mwendokasi hatarishi katika maeneo ya makazi ya watu au yasiyoruhusiwa na alama za barabarani.

"Kongamano la usalama barabarani ni siku muhimu sana ya kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Masuala hayo ni pamoja na kuwakumbusha madereva juu ya kuwa waangalifu na kuzingatia sheria" amesema Simbachawene

Chanzo: Nipashe
 
Hapooo kwenye vitambi sasa sipati picha huyu jirani hapa.
 
Kama kitambi ni kikwazo mcheki huyu baharia.
 

Attachments

  • VID-20191210-WA0019.mp4
    6 MB
Traffic wote wenye vitambi pereka FFU, chukua FFU pereka barabarani. Full stop poti.
 
Ni kweli, lakini sio kila mwenye kitambi ni mnyonyaji au mzembe kazini.
 
Back
Top Bottom