Waziri Simbachawene: Huwezi kumchukua aliyepata divisheni 1 ili akalinde benki au kucheza gwaride, lazima muelewe jamani

Waziri Simbachawene: Huwezi kumchukua aliyepata divisheni 1 ili akalinde benki au kucheza gwaride, lazima muelewe jamani

Tatizo hao failures wanaumiza wasio na hatia, hawazijui sheria za nchi, wao kukamata na kumpiga mtuhumiwa wanaona sifa, hili waziri anatakiwa kuliangalia, sio lazima mpaka polisi awe na digrii ndio ajue mipaka ya majukumu yake.

Wanatakiwa kutoa elimu kwa hao vilaza wajue kumpiga mtuhumiwa akiwa mikononi mwao ni kosa kisheria, wanaweza kushtakiwa na wakikutwa na hatia watakwenda jela, tatizo wanatumia uoga wa watanzania kuwatendea unyama.
 
Amekosea sana....kwa hiyo jeshi la polisi ni kwa ajili ya watu wenye uwezo mdogo...poor him...
Amewadhalilisha sana polisi sijui kama analijua hili...
Poleni PT.
Polisi wana vyuo vyao!
 
Amekosea sana....kwa hiyo jeshi la polisi ni kwa ajili ya watu wenye uwezo mdogo...poor him...
Amewadhalilisha sana polisi sijui kama analijua hili...
Poleni PT.
Wengi wao ni failures huo ndio ukweli hawajadhalilishwa.
 
mbona juz wamehitimu nyota wenye PHD na Masters huko polisi? labda recruitment hii inataka watumia nguvu tu
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema jeshi la polisi haliajiri waliopata divisheni 1 kulingana na majukumu halisi ya askari watarajiwa.

Huwezi kuajiri divisheni one akalinde benki na kucheza gwaride amefafanua waziri.

Chanzo: ITV Dakika 45

Kwa habari kamili fuatilia kipindi
Kwanini mliwasajili ili wakajiunge waje JKT si mngewaambia mapema kabisa kuliko watu waje wajitolee miaka miwili then Ajira zukija mnawatolea nje.
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema jeshi la polisi haliajiri waliopata divisheni 1 kulingana na majukumu halisi ya askari watarajiwa.

Huwezi kuajiri divisheni one akalinde benki na kucheza gwaride amefafanua waziri.

Chanzo: ITV Dakika 45

Kwa habari kamili fuatilia kipindi
Kumbe hii kazi ya upolisi ni ya Kingai ngai sio, daah ccm Sina hamu nanyi ila wenyewe mapolisi wamesikia wakiamua kufanya Kama kamanda Hamza poa tuu.
Kingai=ujinga
 
Wengi wao ni failures huo ndio ukweli hawajadhalilishwa.
Ndiyo maana tunasema kuendelea kuongozwa na watu wale wale, wenye maono yale yale kwa kutumia system ile ile ni wendawazimu na hakuna kitakachobadilika. Kwani kazi ya polisi ni kulinda benki au kucheza kwata? Bila katiba mpya itakayoondoa watu na mawazo mgando kama haya hakuna jipya.
 
Kwa hiyo kazi ya polisi haihitaji weledi, I mean professionalism.......unajengaje professionalism kwa bongolala...
 
Back
Top Bottom