Kuna kijiji kimoja kinaitwa Sanjaranda huko Itigi mkoani Singida nimekuta mnara wa Tigo(yas) unajengwa na mfuko wa mawasilano. Kijiji hicho na vijiji jirani kupata masafa ya redio hasa TBC na nyingine hazisikiki wananchi wanaishi hata hawajui nchi yao inaendaje. Pamoja na mawasiliano ya simu ni bora pia wakafunga mitambo ya kunasa masafa ya redio hapohapo mnarani na makampuni mengine ya simu nao wajenge minara yao hapo. Kuna maeneo mengi ya katikati ya nchi bado hayana mawasiliano ya simu na haya ya fm kwa redio. kupiga simu hadi uende kijiji cha mbali ukapande kichuguu au mti ndio upige simu, hiki ni kituko miaka hii