Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri Tabia Mwita Aipongeza Tanzania Youth Icon (TAYI)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ameupongeza Uongozi wa taasisi ya Tanzania Youth Icon (TAYI) kwa mpango wao wa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Alabama.
Waziri Tabia ameyasema katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa uwanja huo kati ya Taasisi ya TAYI na kampuni ya Sky City katika ukumbi wa skuli ya Dk. Ali Mohammed Shein Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema Uwanja huo utaongeza idadi ya viwanja bora ndani ya Zanzibar ambavyo vitakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kukuza vipaji vyao hivyo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kukamilika ujenzi wa uwanja huo kwa wakati.
Naye Mlezi wa TAYI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewapongeza wafadhili waliochangia katika kuwezesha mpango wa ujenzi huo kuanza kutekelezwa kwani mradi huo utawasaidia vijana wengi wa Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla katika kuendeleza vipaji vyao.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Youth Icon Abdallah Othman Miraji ameiomba Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwasaidia wataalamu wa kuuendeleza uwanja huo baada ya kukamilika kwake ili uwanja huo uendeshwe kwa ufanisi.
Uwanja huo wa Alabama ambao upo katika Jimbo la Kikwajuni utajengwa kwa muda wa miezi 18 na unatarajiwa kugharimu Shilingi Bilioni 1.7 hadi kukamilika kwake
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.00.jpeg50.5 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.00(1).jpeg40.6 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.01.jpeg44.3 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.01(1).jpeg50.9 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.02(2).jpeg44.6 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2023-11-28 at 12.23.02(3).jpeg53.1 KB · Views: 3