Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwa aibu niliyojiskia leo baada ya kusikiza Kiingereza cha Waziri Ulega akizungumza na Wakandarasi Wachina wanaojenga barabara ya mwendokasi huko Mwenge leo nakuomba tu Msemaji wa Serikali zungumza na Waandishi wa habari na waombe tu wasirushe zilr clips za Waziri wetu akizungumza kiingereza.
Kwa kifupi tu Waziri wetu kaharibu mbaya. Ile clip ikienda viral ni aibu sana 😅. Kile kiingereza kitatuaibisha sana kama Taifa. Ni broken isiyovumilika.
Mwisho jamani nafasi za Uwaziri ni kubwa sana. Hawa ni watu wanao negotiate deals kwa faida ya nchi. Wanaosimama kwenye international platforms kuwakilisha nchi. Jamaniii tuteue watu wenye uwezo hata wa kuzungumza hizi lugha kubwa za kigeni kama kiingereza kwa ufasaha.
Poleni Tanzania. Ni aibu