Waziri Ulega akipiga mkwara na Kingereza cha ugoko

Did ikishatumika tu, basi main verb Kama iyo understand inabakia ivyo ivyo.
Nakumbuka mwalimu wangu wa English primary mlimani primary school alisema kuwa Kuna walimu wanamkaririsha mwanafunzi kuwa ukiona yesterday basi go inakuwa went.
Sasa Kuna aina tatu za Sentesi , question, affirmative and negative Sentences.
 
Kama alishindwa kujisimamia kielimu ili ajifunze kiingereza fasaha atawezaje kusimamia public mega project?
Mkuu,

Huoni kwamba kwa Kiingereza chake hichohicho cha manati, Waziri Ulega ameibua issues muhimu kabisa katika Project Management, issues kama za timeline, mpaka issues za diplomasia ya kimataifa ya urafiki wa Tanzania na China ambao kampuni hii inatishia kuuharibu?

Hujaona Waziri Ulega anafanya kitu muhimu kabisa katika Project Management kinaitwa MBWA, Management By Walking Around, anapitia hiyi sehemu kuangalia kama wanafanya kazi mpaka weekend na anaona hawafanyi kazi?

Na ingawa Kiingereza si kizuri sana, kajieleza kuhusu issue hizi na zimeeleweka?

Mkuu,

Huoni kwamba watu wana focus kwenye Kiingereza tu wakati Waziri Ulega ame raise mambo muhimu sana mpaka yanayohusu traffic jams za Dar, na watu hawaongelei haya mambo muhimu, ambayo kabda yameelezwa kwa Kiingereza cha manati, lakini yameelezwa, watu wanaishia kujadili Kiingereza tu?
 
Mbona limeongea kizuri tu kwa size Tanzania aiseee! Wewe cha kwako kiko wapi?
 
Binafsi naona kaongea vizuri, labda na mimi ndio walewale.

Tutofautishe grammatical errors na accent, grammar yake haikuwa mbaya, tena yupo vizuri kuliko wengi wetu. Accent yake ni ya kiafrika, au tunataka aongee kama muingereza?
Hmm really? Mbona amefanya makosa mengi tu ya kisarufi hapo….

Na siyo kakosea kwenye sarufi tu. Hadi syntax katenda makosa kadhaa.
 
Limeongea vizuri bwana tena pronounciation ya lenyewe iko vizuri tu 'we can not allow that!"
 
Mbona mkuu wa mkoa alimsifia kuwa yuko fit sana?
 
Hmm really? Mbona amefanya makosa mengi tu ya kisarufi hapo….

Na siyo kakosea kwenye sarufi tu. Hadi syntax katenda makosa kadhaa.
Inaweza isiwe advanced au proficient, ila ikawa intermediate au upper intermediate mkuu!! Kwa level ya Tanzania na watanzania mimi naona hayupo mbali sana.
 
Sio tu Did bali forms zote za auxiliary verb DO(do,does,did) zikisimama na main verb kwenye sentensi zinabaki katika base form au umbo lake la dictionary ukipenda wengine waziita simple verbs
 
Wewe kweli Zumbukuku wa mwisho usiyejielewa ushawah kumsikia Putin, Xi jinping au Rais wa Iran wakiongea kingereza...Acha utumwa wa Akili Bro.
Kingereza ni lugha tu kama Kipare
 
Mbona kiingereza chake siyo kibaya...tatizo watz na wakenya mnataka mtu aongee kiingereza kama native speaker...hicho kitu hakipo. Cha misingi ni ujumbe kufika na mawasiliano yafanyike..
 
Inaweza isiwe advanced au proficient, ila ikawa intermediate au upper intermediate mkuu!! Kwa level ya Tanzania na watanzania mimi naona hayupo mbali sana.
Kwa viwango vya Watanzania waliosoma mpaka elimu ya chuo, hayuko vizuri, licha ya kwamba mtu unaweza kuelewa alichokuwa anakimaanisha.

Ingawa sina hakika na elimu yake, nahisi walau atakuwa na elimu ya diploma au chuo kikuu.

Uzungumzaji wake naulinganisha na ule wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli na shahada zake tatu ila uzungumzaje wake wa lugha ya Kiingereza ulikuwa mbovu sana.
 
Limeongea vizuri bwana tena pronunciation ya lenyewe iko vizuri tu 'we can not allow that!"
Sawa mkuu, wewe umeshatoka kwenye lugha.

Vipi kwenye substance.

Kuna watu wanasema Ulega muongo, haiwezekani serikali itoe hela yote halafu mkandarasi azembee hivyo.

Ama serikali haijatoa pesa zote, ama kama imetoa pesa zote hata kwenye upande wa serikali ufuatiliaji umezembea.

Kuna mtaalamu mmoja niko naye hapa anasema hivi.

Lazima kampuni Class A itumie hela zake.

Lazima ulipaji uende awamu kwa awamu kila awamu ikikamilika malipo yafanywe.

Serikali kama wamelipa hela zote, kwa nini hawakukagua mradi mpaka mwezi mmoja kabla ya mradi kukamilika?

Kwa nini Ulega anaweka drama nyingi wakati angeweza kusema anavunja mkataba kwa kuwa mkandarasi hajatimiza vigezo hivi na vile vya mkataba?

Hapo vipi?

Huoni kwamba kwa kujikita kwenye Kiingereza cha Ulega (bila kujali ni kizuri au kibaya) tunakosa kujadiliana kwenye haya mambo mengine muhimu sana?
 
Mkuu,Umemtetea na Kumkosoa Kwa Wakati Mmoja ...Msimamo Wako Ni Upi Uko Upande Gani?
 
Ndalichako yule sijui alipata je udakitari PhD, wote na mwendazake kiingereza kinawasumbua na Zelensky wa Ukurain anawaxidi wakati hakusoma kiingereza
Kile cha Ndalichako ni kiboko ukizingatia alikuwa waziri wa elimu.
 
Mkuu,Umemtetea na Kumkosoa Kwa Wakati Mmoja ...Msimamo Wako Ni Upi Uko Upande Gani?

Msimamo wangu ni kudai katiba mpya itakayotupa rais na mawaziri politico-technocrats watakaopanda kwa meritocracy ambao hawatakiwi kutokana na wabunge.

Msimamo wangu ni kukataa false dichotomies.

Hili si jambo la ama kumtetea ama kumkosoa, kuna nuances nyingi hapa. Nyingine ni systemic ambazo zimevuka level ya kawama kwa mtu mmoja, kama hiyo ya katiba mpya hapo juu.

Kama Kiingereza ni muhinu hivyo, kutoka bunge lililojaa wabunge wasiojua Kiingereza vizuri, unategemea vipi rais awe na mawaziri wanaojua Kiingereza vizuri?

Huyu si peke yake. Tumeona Jenister Mhagama alivyohangaika kuongea Kiingereza cha kujitambukisha na diplomasia ndogo za mikutano kule Congo kwenye mkutano wa WHO nafikiri.

Msimamo wangu ni kwamba, ingawa Waziri anatakiwa kujua Kiingereza kizuri, na hana excuse kwenye hilo, huyu ndiye Waziri wetu na hayo ndiyo maneno aliyoyasema. Na huyu kama muwakilishi wa Watanzania, ambao wengi wana matatizo ya Kiingereza, simtegemei ajue Kiingereza cha Received Pronunciation cha BBC.

Kwa Kiingereza chake hicho cha kuunga unga, tunaweza kuelewa kasema nini?

Kama tumeelewa, tunaweza kujadili alichosema badala ya kujadili umahiri wake katika Kiingereza?

Inawezekana mkamlaumu Waziri kutokujua Kiingereza, kumbe lawama ni za rais na wananchi waliomchagua. Ukimchagua mbunge umesema huyu mtu anafaa kuwa waziri dakika yoyote.

Sasa, hao wananchi wanaochagua wabunge wanajali Kiingereza?

Wananchi wanachagua wabunge wanaowataka kweli?

Sasa kama Watanzania wengi hawajui Kiingereza na huyu ndiye muwakilishi wao wanaona anawafaa, kwa kuwa wao kujua Kiingereza si muhimu kama kujua matatizo yao, akiwa waziri kwao ni sawa, hapo kuna kosa?

After all, hata hapa wengi wamesema Kiingereza chake ni cha kawaida tu kwa Mtanzania, na kwamba hata rais Magufuli alikuwa na Kiingereza kama hiki.

Tumejadili hoja alizosema Ulega au tumeishia kwenye Kiingereza tu?
 
Mkuu uchina urusi wajerumani wafaransa wareno mbona wana lugha zao na maisha yanaenda so hawaingiagi miktaba ,yaani mmekuwa brainwashed Ile mbaya
Kwani wao wakiwasiliana kwa kingereza huwa wanapata tabu kama Ulega!!?
Kwani wao wakiingia mikataba huwa wanatumia kiingereza ama wanatumia lugha zao!!??
Kwani wao shule zao wanajifunza kwa kutumia kiingereza ama kwa lugha zao!!??

Muombe Mungu sana akupe akili ya kusoma na kuelewa hoja kwa umakini kabla ya kukurupuka kujibu au kuongea.
 
Mlimani ya Mndolwa!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…