Waziri Ulega akipiga mkwara na Kingereza cha ugoko

Waziri Ulega akipiga mkwara na Kingereza cha ugoko

Eti muulize wewe. Wakati mkandarasi yupo pembeni. Ila jiwe aligoma kutumia English kwa kichaka cha kukuza Kiswahili, ukweli lugha ilikuwa haipandi
Hapana jiwe alikuwa anapenda sana kushirikisha wasaidizi wake ili na wao wajisikie fahari katika maamuzi.Siyo kwamba ngeli ilikuwa haipandi
 
Wachina kiingereza sio lugha yao ila angalia hiyo habari alafu linganisha kiingereza cha mchina na waziri wetu ambaye nchi yetu inakitambua pia kiingereza kama moja ya lugha rasmi.
Hata Watanzania kiingereza siyo lugha yao
 
You have our money ndo kuongea vizuri?😅
This sentence is grammatically sound and entirely free of errors. However, if you, as a language expert, believe otherwise, kindly pinpoint the specific flaw. Moreover, if you perceive a mistake where none exists, it would only indicate that your own command of English is questionable.
Huyo Waziri hapo kaongea kama mtoto wa kindergarten anayeanza kujifunza kiingereza. Anavutaaaa maneno, anakosea maneno wakati yupo kwenye issue serious. No wonder huyo mchina alianza kumcheka🤣🤣🤣
Usikute hata wewe Huwezi kuandika wala kuongea kingereza kilichonyooka.
 
Kingleza hasa cha kugombeza kitakuwa changamoto kwa kweli hata miye siwezi! 😄
Naona Waziri kajitahidi sana!
 
Humu wengi wanaomsema huyo waziri ukiwaambia waandike au kuongea hicho hicho kingereza basi utaishia kusikitika tu ni wachache sana humu wanaoweza kunyoosha kingereza kama cha kina Kiranga, Nyani Ngabu au Prof Griff
Kama Kiingereza ni muhinu, hata hao watu wasiojua Kiingereza wana haki ya kumsema Waziri.

Kwa sababu Waziri ni kiongozi, katafuta uongozi, anategemewa ajue vitu kama hii lugha.

Waswahili wa kawaida ambao hawajaomba uongozi hawalazimiki kujua mambo mengi.

Kuhusu Kiingereza cha Kiranga. Kiingereza changu ni cha kawaida sana, mtu yeyote aliyesoma Newsweek in teenage years atakijua kuwa cha kawaida tu.

Tatizo Watanzania wengi Kiingereza ni mgogoro mkubwa sana mpaka mtu anayeongea na kuandika Kiingereza cha kawaida kabisa kama Kiranga anaonekana anajua sana kwa wengi wao.
 
Mimi sijaona tatizo la kingereza cha waziri...

Amezungumza vizuri na anaeleweka vizuri kabisa...

Ndiyo, kuna changamoto kidogo ktk grammar yake (uundaji wa setensi) na matamshi (pronounciation) yake ambako kuna errors/mistakes za hapa na pale, lakini ktk informal speaking kama hapa, kikubwa tunaangalia kufika na kueleweka kwa ujumbe...

Hapa kila mtu ameelewa, mimi nimemwelewa waziri na haina shaka kuwa waliokuwa wana interact naye wameelewa pia...

Usitegemee mtu yeyote ambaye kiingereza sio lugha yake ya kwanza akawa na ufasaha wa kuizungumza na kuandika kwa 100%. Wote humu ndivyo tulivyo hata kama utajirahidi kwa namna zako zote, lazima utakamatwa na makosa ya kutosha ktk writing au speaking yako...

Kama kuna anayebishia hili kuwa yeye yuko competent & fluent kwenye lugha hii, tupeane mtihani mdogo humuhumu...

Nawahakikishia, kila mtu atashangaa, maana wale wanaomhukumu waziri kuwa hajui kiingereza, tutapigwa na butwaa kujua kuwa waziri Ulega is far better than most of these critics here..!

Waziri is very good, amejitahidi....
Mkuu waziri is very good ulitaka kusemaje/ waziri is very good.
Ni Bora unge andika kwa kiswahili kwamba waziri yupo vizuri kwenye kukiongea/ kuzungumza kingereza.

All in all,
Ukipewa au ukiwa na Nia ya kugombea unatakiwa ujue lugha hilo halina excuses.

Kitendo Cha executive members wa TAIFA kusua sua kwenye kutema yai haina EXCUSES ni Bora wabakie kua common Man kuliko kuli haibisha taifa letu.
 
Kama Kiingereza ni muhinu, hata hao watu wasiojua Kiingereza wana haki ya kumsema Waziri.
You're absolutely correct, Mkuu. While they are within their constitutional rights to criticize the Minister, given that their critique centers on his proficiency in English, it would have been more prudent for them to offer their criticisms in the very same English language, thus allowing for a fair evaluation of their own linguistic competence as well.
Kwa sababu Waziri ni kiongozi, katafuta uongozi, anategemewa ajue vitu kama hii lugha.
I agree with you.
Kuhusu Kiingereza cha Kiranga. Kiingereza changu ni cha kawaida sana, mtu yeyote aliyesoma Newsweek in teenage years atakijua kuwa cha kawaida tu.
Even an individual accustomed to perusing esteemed global publications such as The New York Times, The Guardian, The Economist, or someone well-versed in the writings of distinguished authors, including prominent figures from our country like Jenerali Ulimwengu, would undoubtedly perceive your English as rather basic.
Tatizo Watanzania wengi Kiingereza ni mgogoro mkubwa sana mpaka mtu anayeongea na kuandika Kiingereza cha kawaida kabisa kama Kiranga anaonekana anajua sana kwa wengi wao.
Basi hao walikimbia shule.
 
You're absolutely correct, Mkuu. While they are within their constitutional rights to criticize the Minister, given that their critique centers on his proficiency in English, it would have been more prudent for them to offer their criticisms in the very same English language, thus allowing for a fair evaluation of their own linguistic competence as well.

I agree with you.
Even an individual accustomed to perusing esteemed global publications such as The New York Times, The Guardian, The Economist, or someone well-versed in the writings of distinguished authors, including prominent figures from our country like Jenerali Ulimwengu, would undoubtedly perceive your English as rather basic.
Basi hao walikimbia shule.
Kama Kiingereza ni muhimu, si lazima kujua Kiingereza kuunga mkono hoja ya kusema Waziri kuharibu Kiingereza ni jambo baya.

Inawezekana mtu akaunga mkono hiyo hoja, kwa Kiswahili, hususan kwa sababu yeye hajui Kiingereza.

Mtu asiyejua Kiingereza anaweza kuunga mkono hoja ya umuhimu wa Kiingereza kwa viongozi bila kujua wala kutumia Kiingereza.

Hoja hapa ni umuhimu wa Kiingereza kwa viongozi, sio umahiri wa Kiingereza wa wananchi.

Hoja ya umuhimu wa Kiingereza kwa viongozi si hoja ya mashindano ya kukogana nani anajua Kiingereza zaidi. Msiifanye kuwa hoja ya kukogana nani anajua Kiingereza zaidi.

Mwananchi hahitaji kujua Kiingereza kwa umuhimu ambao kiongozi anahitaji.

Usichanganye mambo mawili haya tofauti.
 
Kwanini watu wasio jua kiingereza wanaongea tena kwa sauti kubwa huyu mzee kiingereza hakijui preposition zake ziko poor, pronunciation poor grammar poor eti ni waziri wa ujenzi, hi nchi ina kasoro kubwa katika uongozi.
Asipojua kiìngereza kwa ufasaha atashindwa kuongoza na kusimamia miradi? ,english is not aparameter for measuring intelligence
 
Mkuu waziri is very good ulitaka kusemaje/ waziri is very good.
Ni Bora unge andika kwa kiswahili kwamba waziri yupo vizuri kwenye kukiongea/ kuzungumza kingereza.

All in all,
Ukipewa au ukiwa na Nia ya kugombea unatakiwa ujue lugha hilo halina excuses.

Kitendo Cha executive members wa TAIFA kusua sua kwenye kutema yai haina EXCUSES ni Bora wabakie kua common Man kuliko kuli haibisha taifa letu.
Wewe unaweza kuandika au kuzungumza Standard English Language kwa ufasaha? Je, si kwamba unakijua kilekile tu cha kujikanyaga kanyaga kama tu ambavyo Waziri anakijua ..?

It's very simple to examine you, and therefore nataka tukupime sasa hivi hapa....

Can you translate hiki ulichoandika hapa kwa kiswahili kiwe ktk lugha ya Kiingereza...?

Nataka tukisome chako...

All in all, nina hakika wa jambo moja kutokea ukikubali kufanya mtihani huo☝🏻☝....

Kwamba, chako chaweza kuwa cha hovyo zaidi kuliko cha Waziri Ulega....

Kwanini unadhani?

JIBU NI RAHISI SANA:

➡Kwamba, always hakuna perfection ya 100% ktk lugha yoyote hata kama ni kiswahili ambayo ni lugha yako mama, sembuse kiingereza lugha ya pili ya kujifunza ukubwani..!?

➡Lugha ni namna tu ya kuwasiliana na wenzako ili mpate kuelewana, shughuli zifanyike na mahusiano ya kijamii yaendelee...

➡Sasa niambie wale Wachina unadhani hawakumwelewa Waziri Ulega kwani...?
 
Hoja hapa ni umuhimu wa Kiingereza kwa viongozi, sio umahiri wa Kiingereza wa wananchi.
Binafsi kwa hali ya kawaida sioni kama huyu kiongozi hajui kuongea kingereza kama wanavyomkebehi hapa lakini anakosa kitu kinachoitwa "Speaking Fluency" na hilo ni jambo la kawaida kwasababu kingereza sio lugha yake ya kwanza na pengine ni lugha yake ya tatu kabisa.
 
Kiingereza cha Waziri, katika nchi ambayo Kiingereza ni lugha rasmi, si kizuri, huwezi kukitetea.

Na pengine kama hujazoea Kiingereza kizuri, huwezi kuona mapungufu.

So, from the outset Ulega kakosea, aliyemteua Ulega kakosea. Hilo kwangu halina mjadala. Waziri anatakiwa kujua Kiingereza. Akisafiri nje ataongea Kiswahili? Hata kama atatafsiriwa, kama Kiingereza chake cha matata, ataweza kusoma na kuelewa mambo ya nje ya Tanzania? Kutokujua Kiingereza, hata kama kuna watafsiri, kunapunguza efficiency ya mawasiliano.

Hiki Kiingereza angeongea Waziri wa DR Congo, ningeweza kumtetea kuwa nchi yao hawaongei Kiingereza. Lakini kwa nchi ambayo Kiingereza ni lugha rasmi, Kiingereza hiki si kizuri, lakini pia si Kiingereza fulani ambacho hakieleweki Waziri anasema nini.

Sasa hapo tunapaswa kujiuliza swali.

Of course in the perfect world tunatakiwa kuwa na Waziri anayejua Kiingereza vizuri na anayewabana anaotakiwa kuwabana kwa Kiingereza kilichonyooka kabisa.

Lakini je, ukiwa na Waziri kama Ulega mwenye Kiingereza cha kuvuta kwa manati, ungependa afanye nini? Asifanye kazi yake ya kuwabana anaotaka kuwabana mpaka aweze kuongea Kiingereza cha Mfalme Charles kwa lafudhi ya Received Pronunciation ya James Naughtie wa BBC?

Labda vijana wa sasa hamjui habari ya Bunge la Tanzania kuanza kukubali Kiswahili ilianzaje.

Mbunge wa Kinondoni ( nafikiri Kinondoni), Bibi Titi Mohammed, alikuwa bungeni akitaka kuwakilisha watu wake vizuri, akitaka kudai umeme upelekwe Magomeni watu wa Magomeni wafaidi kuwa na taa za umeme.

Lakini Bibi Titi Mohammed, ingawa alikuwa na ari kubwa sana ya kuwasilisha hoja yake hii bungeni, hakuwa msomi, hakujua sana Kiingereza.

Bibi Titi Mohammed akawa na uamuzi mgumu sana. Je, asimame na kudai anachotaka kudai kwa Kiingereza ambacho hakijui vizuri na anaweza kuboronga maneno akachekwa na watu? Au akae kimya na kuogopa kuharibu Kiingereza, lakini kwa kukaa kimya hivyo, aiachie nafasi ya kupigania haki za wananchi waliomtuma bungeni?

Bibi Titi Mohammed akaamua kusimama na kuongea kwa Kiingereza hicho hicho cha manati alichokijua.

Hapo ndipo aliposimama na kutoa hotuba iliyopata umaarufu ya "fire in the bottle". Akisema kwamba "We want fire in Magomeni...We want fire in small bottles".

Watu wakawa hawaelewi, anamaanisha nini kwa kusema "We want fire in small the bottles"?

Wakaja kugundua kuwa alikuwa anadai umeme ili watu wa Magomeni wapate taa za umeme, "fire in small bottles" ni zile taa za umeme.

Sasa hapo utamcheka Bibi Titi kuwa alikuwa hajui Kiingereza? Au utamsifia kuwa huyu alikuwa shujaa wa kupigania maslahi ya wananchi waliomtuma, hata pale ambapo hakujua Kiingereza vizuri, alisimama hivyohivyo ili nradi kawakikisha watu wake tu?

Serikali ililiona hili tatizo. Watu wetu wengi hawajui Kiingereza, kwa nini tunalazimisha bunge liwe la Kiingereza?

Wakabadilisha mfumo wakaruhusu wabunge kuongea Kiswahili.

Ulega kaharibu lugha. Hapo siwezi kumtetea.

Vipi kuhusu substance?

Kuna watu wamezungumzia substance ya alichoongea Ulega?

Au tumeishia kucheka lugha tu?
 
Asipojua kiìngereza kwa ufasaha atashindwa kuongoza na kusimamia miradi? ,english is not aparameter for measuring intelligence
Kama alishindwa kujisimamia kielimu ili ajifunze kiingereza fasaha atawezaje kusimamia public mega project?
 
Kwa aibu niliyojiskia leo baada ya kusikiza Kiingereza cha Waziri Ulega akizungumza na Wakandarasi Wachina wanaojenga barabara ya mwendokasi huko Mwenge leo nakuomba tu Msemaji wa Serikali zungumza na Waandishi wa habari na waombe tu wasirushe zilr clips za Waziri wetu akizungumza kiingereza.

Kwa kifupi tu Waziri wetu kaharibu mbaya. Ile clip ikienda viral ni aibu sana 😅. Kile kiingereza kitatuaibisha sana kama Taifa. Ni broken isiyovumilika.

Mwisho jamani nafasi za Uwaziri ni kubwa sana. Hawa ni watu wanao negotiate deals kwa faida ya nchi. Wanaosimama kwenye international platforms kuwakilisha nchi. Jamaniii tuteue watu wenye uwezo hata wa kuzungumza hizi lugha kubwa za kigeni kama kiingereza kwa ufasaha.

Poleni Tanzania. Ni aibu
Bado unayo slavery mindset.
Mbona wachina hawaongei English Ila wanafanya mambo makubwa mno.
Ndio mana mnalipia mamilioni makubwa ili tu mtu aongee ama ajifunze English ni ulimbukeni mkubwa ndio nyie mkienda kwa wazungu mnajiona na nyie mmekuwa wazungu ama ni mafanikio.
Ishu ni kichwani unamiliki nini, unajua nini ,mbona English ni sawa tu na kirusi ,kipoland, kisukuma, unadhani mtu akijua English basi ndio ataweza Jenga daraja kubwa ama kufanya hesabu.
English is immaterial
 
Mi sijui tutatibu vipi hili tatizo kwa kweli. Mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo anashindwa kuunganisha sentensi tatu za kiingereza
Ni hatari sana. Kuna mahali hakuko sawa kwenye mfumo wetu wa elimu. Chuo kikuu unakuta mwanafunzi anapresent kwa Kiswanglish mwalimu nae vivo hivyo. Kwa tunapoelekea, graduates wetu watashindwa kushindana kwenye soko la ajira la kimataifa kwa sababu hawataweza kufaulu interview.

Tumeweka siasa kwenye kila kitu, sasa elimu yetu imekua ya ajabu, tuna graduates wenye ujasiri wa kuita Media kupinga kuajiriwa kwa interview, why? Kwa sababu hawajui vitu na wengi hawawezi kujieleza tena kwa kiingereza.

All in all, ukiwa na mwanao, hakikisha pamoja na kujua Kiswahili, awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika kiingereza vizuri. Itamsaidia sana.
 
ukijumlisha na lugha ya kiingereza kwani ndio wanaoingia mikataba kwa niaba ya wizara na nchi.
Mkuu uchina urusi wajerumani wafaransa wareno mbona wana lugha zao na maisha yanaenda so hawaingiagi miktaba ,yaani mmekuwa brainwashed Ile mbaya
 
Ni hatari sana. Kuna mahali hakuko sawa kwenye mfumo wetu wa elimu. Chuo kikuu unakuta mwanafunzi anapresent kwa Kiswanglish mwalimu nae vivo hivyo. Kwa tunapoelekea, graduates wetu watashindwa kushindana kwenye soko la ajira la kimataifa kwa sababu hawataweza kufaulu interview.

Tumeweka siasa kwenye kila kitu, sasa elimu yetu imekua ya ajabu, tuna graduates wenye ujasiri wa kuita Media kupinga kuajiriwa kwa interview, why? Kwa sababu hawajui vitu na wengi hawawezi kujieleza tena kwa kiingereza.

All in all, ukiwa na mwanao, hakikisha pamoja na kujua Kiswahili, awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika kiingereza vizuri. Itamsaidia sana.
Kuna namna CCM wameifelisha hii nchi hakuna namna tunaweza wasamehe.
 
Back
Top Bottom