Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Kilimo na Mifugo, Abdallah Hamis Ulega ameyasema hayo wakati alipomuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko kwenye Mkutano wa 52 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya uliofanyika Kitonga, Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Amesema Mkutano huo umeandaliwa vema na unajadili wito wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu viongozi wa Dini kujadili masuala ya suala la mmomonyoko wa maadili na hatua za kufanya ili kuondoa changamoto hiyo.
Ameeleza kuwa mafundisho ya Dini yapo wazi na yanaweza kusaidia kuepusha suala la kuzuia mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza wakati wa Mkutano wa 52 wa Jalsa Salana ambao ni mkutano rasmi na wa kila Mwaka wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya. Tukio hilo lilifanyika katika Kijiji cha Msongola, Kata ya Msongola, wilayani Ilala.
“Watu wanatakiwa kurejea katika mafunzo ya Dini ili kuzuia changamoto zinazojitokeza, kutumia viboko peke yake, kutumia Sheria za Binadamu kunaweza kusiwe na msaada wa kila kitu japokuwa ni muhimu na vinatakiwa kuendelea kutumika.
“Mila na Desturi zetu ni pamoja na Dini ambazo zinafunza Watoto tangu wakiwa wadogo, wajue kuwa kumchukia mtu ni haramu,” amesema Naibu Waziri wakati wa siku ya mwisho ya mkutano huo wa Siku Tatu.
Ameongeza kuwa upole, mapenzi na mapenzi kwa watu ni mila nzuri na zinapokosekana ndio chanzo cha matatizo mbalimbali.
Kauli Mbiu ya Mkutano huo huo ilikuwa ni 'Tawheed ya kweli haiwezi kusimamishwa bila ya Ukhalifa', ikielezwa maana yake ni mfumo wa Ukhalifa ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za Nabii Adam ndio njia pekee ambayo Mwenyezi Mungu Hudhihirisha Umoja wake Duniani na leo hii Tawheed ya kweli itasimamishwa kupitia Ukhalifa ulioanzishwa tena na Mwenyezi Mungu katika Uislam sawa na ahadi iliyotolewa na Mtume Muhammad s.aw.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry ambaye ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Tanzania katika Mkutano wa Jumuiya hiyo, eneo la Ahmadiyya Centre lililopo Kitonga, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Ghana
Naye, Muhammad bin Salih ambaye ni Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Ghana aliyeshiriki kwenye kutano huo amesema licha ya kwamba mkutano husika haujashirikisha idadi kubwa ya washiriki kama ilivyo katika Nchi nyingine ikiwemo Ghana lakini ameona kuna nidhamu kubwa ambayo ni sawasawa na inayopatikana kwingine kote.
Ameeleza kuwa ushiriki wa mamlaka za juu za Serikali inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Ahmadiyya na Serikali ya Tanzania.
“Nimemuona Waziri amekuja hapa, amekuwa huru, ametoa hotuba nzuri n ahata mahojiano aliyofanya na Wanahabari nayo yanaonesha utayari wa mamlaka katika kushirikiana na jamii yetu,” amesema na kuongeza:
Mkutano wa Jalsa Salana
Akielezea kuhusu mkutano huo ambao pia unafahamika kwa jina la Jalsa Salana, amesema unazungumzia kuhusu maisha na vintu ginvine vingi vinavyofanyika kwenye jamii ya Ahmadiyya na watu wengine tofauti.
Jalsa Salana hufanyika katika kila nchi ambapo Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ipo.
Amesema “Uzuri wa Mkutano huu unawashirikisha watu wa dini zote kwa kuwa lengo ni kuwafanya watu kuwa karibu na Mungu.”
Ameeleza Utaratibu wa kufanyika kwa Jalsa Salana ulianzishwa na Mwanzilishi mtukufu wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. kwa malengo ya kuwapatia waumini fursa ya kukuza udugu, maelewano mema na ufahamu wa pamoja miongoni mwao.
Kuhusu Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya
Ni Jumuiya ya kimataifa inayopatikana kwenye zaidi ya Nchi 212 Duniani ikiwa chini ya kiongozi mmoja (Khalifa mtukufu).
Lengo kuu ni kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam Duniani kote na kuwa mstari wa mbele katika kupinga maana zisizo sahihi zinazonasibishwa na mafundisho ya Uislam kama vile dhana potofu za ugaidi na misimamo mikali isiyovumilia wengine. Pia Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya inajitahidi kupambania amani duniani kote.