Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema watakaohitaji kutumia Daraja la JP Magufuli kwa ajili ya kupiga picha au kurekodi video za muziki watalazimika kuomba kibali Wizara ya Ujenzi kupitia Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza.
"Hatutakataza kufanya kazi zozote za kijamii kama vile kupiga picha au kurekodi kwaya, lakini ni muhimu kuomba kibali kutoka wizara ya ujenzi. Tuna Meneja wa Tanroads atakayeshughulikia utoaji wa vibali hivyo," amesema Ulega.
Mzilankende angekuwepo asingekubali upumbavu huu!
Yaani picha tu?...
Kwani wamejenga kwa hela zao kutoka mfukoni?...
Jamani hii si ni mali ya wananchi?...
inawezekana yuko sahihi sema jinsi habari inavyoletwa, kupiga picha au sijui video ina maana kufunga daraja na kuchelewesha wengine kwa sababu zako binafsi, haipaswi kuruhusiwa …