Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Wameanza kuingiza siasa katika hili tena
 
Kuondoa utata basi waajiri kwa kigezo cha GPA, aliyepata kubwa ndiyo aanze mpaka cut off itakapoishia maana hapo hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa.

GPA ya Zion na GPA ya DUCE je zinafanana? Kuwa na GPA kubwa sio kigezo cha uwezo kazini.
 
Vigezo vifuatavyo vitasaidia kuondoa malumbano ambavyo ni;

1. Waliokaa muda mrefu bila ajira mfano aliyemaliza 2015 apewe kwanza kabla ya alomaliza 2019 maana hata kukaa mtaani tu uzoefu.

2. Ufaulu wa GPA waweke benchmark ya 3.8
Kwenye GPA mie nakazia.
 
Matatizo wanayatengeneza wenyewe

Kosa la kwanza ni ishu ya kuomba (OTEAS) wakati zamani haikuwa hivyo; hii inawapa nafasi watu kupata cha kusema (malalamiko) au kupata cha kufanya (janjajanja)

Kosa la pili ni kuweka kigezo cha kujitolea wakati hamna utaratibu imara wa kutambua walio/ wanaojitolea; bora kidogo vile walikuwa wanaangalia ufaulu ilikuwa angalau lakini kwa hili la sasa hakuna namna ya kuyakimbia wala kukwepa hayo mnayoyalalamikia

Kosa la tatu ni kuchelewesha hizo ajira; Ilitakiwa zitolewe fasta (kama zipo) ili hili lipite watu wabaki kuangalia (kusema) lingine kulikoni kulifanya gumzo kila siku jambo hilohilo wakati lenyewe ni ishu ya watu wachache tu

Toeni ajira or otherwise... mna jambo lenu
 
Kujitolea ndo sifa ya kuajiriwa serikali Kijitolea ndo kigezo cha mtu kuajiriwa serikalini mbona tangazo halina hicho kigezo kwa kweli CCM nchi imewashinda
 
GPA ya Zion na GPA ya DUCE je zinafanana? Kuwa na GPA kubwa sio kigezo cha uwezo kazini.
Kuna kitu kinaitwa standards na ndio maana ukisema upper second inaeleweka ni 3.5 and above vilevile ipo tume ya vyuo vikuu Tanzania.
 
Kuna Criteria za kuweka ila ziwe Liqudity kujitolea, Mwaka wa kumaliza, Masomo ila sio GPA hiyo mtu awezi nyumburika ukiweka Cut Off maanayake kuna watu wanakosa sifa milele ni vyema ungewaambia hilo wakiwa wajaanza shule kabisa.
Inafahamika kwamba ukifaulu vizuri unajiweka sehemu nzuri zaidi.

Vijana wakiwa vyuo lazima msome sio show off tu kila weekend.
 
Kuna kitu kinaitwa standards na ndio maana ukisema upper second inaeleweka ni 3.5 and above vilevile ipo tume ya vyuo vikuu Tanzania.
Mimi si Mwalimu,lakini nashauri wasiangalie GPA. Wakitaka kuangalia hilo basi itawapasa waanalie na ranking ya vyuo.

Kuna vyuo kupata GPA ya 3.9 siyo issue kubwa ila kuna vyuo kupata tu hiyo 3.0 ni shangwe.
 
Yes wakiangalia GPA pia waangalie na vipaumbele vya Vyuo ubaya ubaya tu vyuo kama
UDOM, UDOM vipewe kipaumbere
 
Kuondoa utata basi waajiri kwa kigezo cha GPA, aliyepata kubwa ndiyo aanze mpaka cut off itakapoishia maana hapo hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa.
Kigezo kizuri ni hiki cha kujitolea. Badala ya hicho cha GPA kubwa za kwenye makaratasi! halafu mkikabidhiwa darasa kufundisha, mnaishia tu kujikanyaga na kujimwambafai! Huku content ikiwa ni 0!
 
Swala la kujitolea si sababu ya kumwajiri mtumishi, kwani shule nyingi zilikuwa zinakataa hata kupokea walimu wa kujitolea!! Na waliokubali walikuwa wamepokea walimu wenye udugu na ama waliopo au anafahamika kwa namna fulani.!!!!
 
Huwa nawaza hivi na mie, kuepusha lawama na migogoro.
Tamko limeshatolewa. Wa kujitolea watapewa kipaumbele. Hii ishu ya GPA kubwa ina walakini. Wengine wana GPA kubwa kwa kupitia njia isiyo rasmi ya kuwafurahisha Wakufunzi wao.
 
Amesema kigezo kikubwa kitakachotumika ni hicho akiongeza kuwa, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka.

Duh.....Kiukweli kama taifa tuna changamoto kubwa. Tunajitahidi kuweka pamba masikioni lakini uhalisia utatuumbua.

Ukosefu wa ajira inabidi iwe emergency ya kitaifa!
 
Swala la kujitolea si sababu ya kumwajiri mtumishi, kwani shule nyingi zilikuwa zinakataa hata kupokea walimu wa kujitolea!! Na waliokubali walikuwa wamepokea walimu wenye udugu na ama waliopo au anafahamika kwa namna fulani.!!!!
Ni Shule za wapi hizo zilizokataa walimu wa kujitolea? Mbona walimu wengi walipokelewa?
 
Kwakweli Waziri Ummy ni tatizo sana kuhusu matamko yake anayoyatoa, yanakuwaga na ukakasi fulani hivi!!

Kwani Serikali imeshawai kutangaza hapo awali kuwa walimu waende wakajitolee kufundisha kwasababu wakati wa kutoa ajira wataanza na wanaojitolea??. Haya ni mambo ya ajabu sana, Waziri Ummy cha kuwabagua watu!!

Cha msingi fuateni qualification zinazotakiwa, wekeni criteria ambazo sio biaise otherwise mnataka watu waongee.

Ushauli; Waziri Ummy jitahidi kutoa matamko yasiyokuwa na mkanganyiko. Otherwise, nakupongeza kwa kazi nzuri.
 
Ni Shule za wapi hizo zilizokataa walimu wa kujitolea? Mbona walimu wengi walipokelewa?
Wewe ni mwalimu

Kati ya shule 5 utazoenda shule 4 hazikubali ombi lako...Calculate shule 3 tu ambazo ndio unauwezo wa kuenda bila kupanda gari zimekataa unapata ya 5 lazima upande gari.

Suala hili serikali sijui hawalijui...waweke kigezo cha kujitolea alafu ukienda Shuleni unakataliwa si upumbavu huu.
 
Ni Shule za wapi hizo zilizokataa walimu wa kujitolea? Mbona walimu wengi walipokelewa?
Mimi ndie mwathirika wa hilo na nathibitisha kutokupokelewa kwenye shule zaidi ya tano! sababu zao ni hawana nafasi ila kwa mbali waliopo humo ndani ukikutana nao, wanadai eti wakuu wanaogopa "system"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…