Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

mkuu internship inaenda sanjari na allowances kama busfare, meals and accomodation na ipo kisheria kwa taaluma kama utabibu, unesi, maabara na mafamasia kwa ngazi ya shahada hapa nchini. Vipi hawa walimu mliwatangazia lini wajitolee na ajira zao zinatolewa kwa mfumo huo tangu lini? nani alikuwa anawalipa pesa za kujikimu? na vipi kuhusu taasisi za uma zilizokataa kupokea vijana wa kujitolea?
 
Tatizo ni kubwa kuliko hata ajira zenyewe, boresheni sekta binafsi wau wajiajiri
Kila mmoja anataka aaijiriwe serikalini. Hao walioomba serikalini asilimia kubwa wana ajira tayari shule binafsi na wanalipwa vizuri lakini hawazithami.
 
Hii habari ya Wanaojitolea nayo ni kichaka kingine. Wanaojitolea wenyewe wamepewa nafasi hizo za kujitokea kwa kujuana, then hao hao ndio watakaopewa kipaumbele kwenye kuajiriwa! Hawa masikini wenye hali tete na walioshindwa kujitolea kwa sababu ya kukosa namna ya kujikimu wawapo majitoleoni, itakuaje kwa upande wao?

TAMISEMI wawe fair katika hili. Watumie vigezo vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria.
 
Wewe unadhani ni asilimia ngapi ya wahitimu wanamudu hali ya kujikimu wenyewe pindi wawapo majitoleoni?
 
Huu Ni unyanyasaji unatumiaje kujitolea kuwa kigezo Cha kumwajili mwalim? Sio sawa kabisa . Mtu ajitolee wakat hakuna nauli,hela ya malaz au fedha kwa ajili ya matumiz mengine,anawezaje? Ataishije? Hiki kigezo kinafaa kifutiliwe mbali kabsa
 
Vigezo vifuatavyo vitasaidia kuondoa malumbano ambavyo ni;

1. Waliokaa muda mrefu bila ajira mfano aliyemaliza 2015 apewe kwanza kabla ya alomaliza 2019 maana hata kukaa mtaani tu uzoefu.

2. Ufaulu wa GPA waweke benchmark ya 3.8
Mkuu GPA ya 3.8 ST JOSEPH ni sawa na 3.8 MZUMBE? Kwa wewe unavyodhania?
 
UKWELI MCHUNGU UKIONA KAZI YAKO WAFANYAKAZI MLIOPO NCHI NZIMA NI WENGI KUANZIA ELFU 20 BASI MSHAHARA WENU LAZIMA UWE MDOGO.
 
Wewe unadhani ni asilimia ngapi ya wahitimu wanamudu hali ya kujikimu wenyewe pindi wawapo majitoleoni?
Mkuu ukijitolea kijijini kwenu ulikozaliwa au kwenye shule ya mtaani kwenu unagharamika nini- mbona mkiitwa na Mbowe kwenye maandamano mnaenda na kudai hamulipwi kitu wala kusombwa kama wale wa CCM- unakera sana wewe na kijilizaliza kwako.
 
Mkuu ukishatangaziwa hiyo ni ajira sasa- kujitolea unajipeleka
 
Mkuu ukijitolea kijijini kwenu ulikozaliwa au kwenye shule ya mtaani kwenu unagharamika nini- mbona mkiitwa na Mbowe kwenye maandamano mnaenda na kudai hamulipwi kitu wala kusombwa kama wale wa CCM- unakera sana wewe na kijilizaliza kwako.
Huna akili
 
Sometimes kusoma sana au kutosoma hakudetermine GPA kubwa.

Huko "Private" vyuo vingi wanapeana miGPA mikubwa mikubwa tu wakati vyuo vingi serikalini wanafunzi wana kazi ya kuoneshana umwamba na ma-lecturerers.
Ooh yes!!!.Umeongea vyema kabisa.

Naona suala la GPA vyuoni ni changamoto sana hasa ukizingatia kuwa kuna baadhi ya vyuo hasa private universities GPA zinatolewa kama njugu.

Next time nitaleta hapa JF special uzi tu jinsi gani kuwe na uwiano wa utoaji wa hizi GPA vyuoni. Je should there be a regulatory body kusimamia hili la GPA, je mitihani ya universities zote isahihishwe na taasisi moja? ....n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…