peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.
Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.
Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.
Mh.ummy mwalimu. Mfumo wa ajira TAMISEMI usiwe wa kupokea maombi ya kazi na kuajiri tu. Ni muhimu wajibu maombi ya waombaji kupitia mfumo huo huo,ili mtanzania aliyeomba ajue kwanza maombi yake yalifika na kupokelewa.
Pili ajue alikosa na sababu za kukosa ili next time akiomba asikose tena akishajua kilichofanya akakosa awali.
Tatu, aliyepata ajue sababu za kupata ilinaweze kuelimidha wengine wasiopata na wanaotarajia kuomba ilu wapate
Mwisho, mfumo wa ajira umekuwa ukifanya kazi kama mfumo wa Siri wa kupata kazi serikalini.