Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.

Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.

Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.

Mh.ummy mwalimu. Mfumo wa ajira TAMISEMI usiwe wa kupokea maombi ya kazi na kuajiri tu. Ni muhimu wajibu maombi ya waombaji kupitia mfumo huo huo,ili mtanzania aliyeomba ajue kwanza maombi yake yalifika na kupokelewa.
Pili ajue alikosa na sababu za kukosa ili next time akiomba asikose tena akishajua kilichofanya akakosa awali.
Tatu, aliyepata ajue sababu za kupata ilinaweze kuelimidha wengine wasiopata na wanaotarajia kuomba ilu wapate
Mwisho, mfumo wa ajira umekuwa ukifanya kazi kama mfumo wa Siri wa kupata kazi serikalini.
 
Habari ya kuajiriwa waliojitolea tu sio nzuri kabisa. Yani ajira hakuna halafu mtu uende ukajitolee badala ya kutafuta njia nyingine mbadala ya kutoka kama kujiajiri na kwenda kujitolea nje ya fani yako. Kama hao 89,000 wote wangejitolea je wangetosha kwenye vituo? Serikali wawe na kigezo bora cha kuajiri na sio chenye upendeleo au ubaguzi wa aina hii. Hii sio fair kabisa.
 
Kuondoa utata basi waajili kwa kigezo cha GPA aliyepata,kubwa,ndiyo aanze mpaka cut off itakapoishia maana hapo hakuna atakayelalamika kuwa,ameonewa.
Hakujawahi kutokea utaratibu huu Serikalini wa kuajiri kwa GPA acha ujinga
 
Huu ujinga ni Tanzania tu, kwa sheria ipi? Ni lini serikali iliwataka wahitimu wakajitolee na malazi na posho ya kujikimu nani aligharamia? Huu upumbavu utengenezeni tu ipo siku mtafurushwa kwa maandamano na riots.
Kujitolea nayo inakuwa sifa ya mtu kuajiriwa? Tunakoenda siko kabisa. Vijana wahamasishwe kufanya kazi za kuwaingizia kipato hata kama ni kidogo, kuliko kuwahamasisha kujitolea.
 
Ninashauri, walioomba na wakakosa ni vema wakajibiwa kwamba wamekosa na wakapewa sababu za kukosa, waliopata vile vile wajibiwe kuwa wamepata na sababu za kupata kuliko ukimya uliopo, unafanya mamilioni ya watafuta kazi kulalamika mitaani.

Pili, mfumo huo uangalie gender pia, kuna uwezekano kuajiriwa gender moja tu. Kwa ujumla mfumo wa ajira uangalie mikoa, wilaya, dini, umri, ufaulu, wenye mikopo, yatima, uwezo wa kifamilia, masomo yenye manufaa kwa sasa, ulemavu, uraia, nk.
Aise hadi dini iangaliwe? Au unasema walimu wa mafunzo ya dini?
 
Vigezo vifuatavyo vitasaidia kuondoa malumbano ambavyo ni;

1.Waliokaa muda mrefu bila ajira mfano aliyemaliza 2015 apewe kwanza kabla ya aliomaliza 2019 maana hata kukaa mtaani tu uzoefu.

2.Ufaulu wa GPA waweke benchmark ya 3.8
GPA sio liqudity kwamaana hiyo chini ya 3.8 ndio kusema haajiriki yeye na serikali basi.

Umewaza hiko
 
Kujitolea nayo inakuwa sifa ya mtu kuajiriwa?Tunakoenda siko kabisa.Vijana wahamasishwe kufanya kazi za kuwaingizia kipato hata kama ni kidogo, kuliko kuwahamasisha kujitolea.
Utumwa mamboleo huo, halafu sekta binafsi wakiiga huu ujinga Serikali inawakalia kooni.
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido Kiruswa aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea. Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo.

Amesema kigezo kikubwa kitakachotumika ni hicho akiongeza kuwa, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka.
========

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.

Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.

Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.

Huu nao ni uongo mtupu... je hao 89 wote wangekuwa wamejitolea wange wapa ajira?
Ni wazi mfumo wa kuajiri tamisemi una makosa mengi sana na ni mfumo unao toa nafsi ya kuwepo kwa upendeleo kabisa.

Ni vyema serikali ikaendelea kutumia mfumo wa ajira portal ili watu wote waitwe wafanyiwe usaili wa kuandika, vitendo na ana kwa ana.......
Huu mfumo wa kujajiri kwa kujitolea unazalisha nafasi ya kuwapendelea watu
 
GPA sio liqudity kwamaana hiyo chini ya 3.8 ndio kusema haajiriki yeye na serikali basi.

Umewaza hiko
Huwezi kuajiri wote lazima utengeneze criteria ndio maana miaka ya nyuma walimu walikuwa wanaajiriwa automatic kwakuwa nafasi zilikuwa nyingi kwasasa mambo yamebadilika.

Survival for the fittest
 
Huu nao ni uongo mtupu... je hao 89 wote wangekuwa wamejitolea wange wapa ajira?
Ni wazi mfumo wa kuajiri tamisemi una makosa mengi sana na ni mfumo unao toa nafsi ya kuwepo kwa upendeleo kabisa.

Ni vyema serikali ikaendelea kutumia mfumo wa ajira portal ili watu wote waitwe wafanyiwe usaili wa kuandika, vitendo na ana kwa ana.......
Huu mfumo wa kujajiri kwa kujitolea unazalisha nafasi ya kuwapendelea watu
Mass Employment ufanyishe Interview is it Thinking...
 
Huwezi kuajiri wote lazima utengeneze criteria ndio maana miaka ya nyuma walimu walikuwa wanaajiriwa automatic kwakuwa nafasi zilikuwa nyingi kwasasa mambo yamebadilika.

Survival for the fittest
Kuna Criteria za kuweka ila ziwe Liqudity kujitolea, Mwaka wa kumaliza, Masomo ila sio GPA hiyo mtu awezi nyumburika ukiweka Cut Off maanayake kuna watu wanakosa sifa milele ni vyema ungewaambia hilo wakiwa wajaanza shule kabisa.
 
Loooo mwendazake ameifikisha hiii jamuhuri pahala pa ovyo na pa ajabu haijapata kutokea.
 
Kuondoa utata basi waajiri kwa kigezo cha GPA, aliyepata kubwa ndiyo aanze mpaka cut off itakapoishia maana hapo hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa.
Kigezo cha haki ni kufuata muda wa kuhitimu masomo yao ya chuo. Kigezo hiki kinazingatia utu. Hapo kila mtu atakuwa na matumaini kuwa zamu yake siku moja itafika.
Suala la kujitolea ni kuwaonea! Ataishije wakati anajitolea?
 
Ajira 7000 tu katika population ya 60m lakini kila siku bungeni mjadala ni huo huo hii ni big deal kweli?!
Bangi tuu na kuonesha kushindwa kwa sera ya kutatua ajira.

Safi Sana maana ilizoeleka tusio walimu ndio tunakuwa na turn out kubwa kwenye usaili,na huku kwingine sasa sifa ya kwanza ni kujitolea na huo ni usaili tosha.
 
na wale walioshindwa kujitolea kutokana na mazingira magumu yalio nje ya uwezonwa? kwa mfano huyo huyo aliyetaliwa ajitolee alikuwa hana uwezo wa kuwa kila siku anaenda ilihali hana matumizi ya kujikimu hivo analazimika kufanya vibarua ajikimu kimaisha na huenda anategemewa na familia yake au yeye mwenyewe anajitegemea.muda sio rafiki angeenda saa ngap kupata ugali na saa ngap kujitolea.je hana nafasi? mazingira hayakua mazuri kujitolea je ?
 
Back
Top Bottom