Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Mimi si Mwalimu,lakini nashauri wasiangalie GPA. Wakitaka kuangalia hilo basi itawapasa waanalie na ranking ya vyuo.

Kuna vyuo kupata GPA ya 3.9 siyo issue kubwa ila kuna vyuo kupata tu hiyo 3.0 ni shangwe.
Watu wengi wanahisi mtu anakua bora kwa chuo alichosoma kwa 3 years tu na kusahau miaka mingine uliyopata elimu kabla ya chuo.
 
Ajira 7000 tu katika population ya 60m lakini kila siku bungeni mjadala ni huo huo hii ni big deal kweli?!
Hii nchi miaka 20 mbele itakuja kuwaka moto kwa maandanano makubwa sana.

Wakati huo hakuna atakayesubiri kuhamasishwa na mwanasiasa. Ni njaa tu itawatoa ndani watu.

Watanzania ni kondoo, lakini hata paka ukimfungia kwenye chumba ukaanza kumpiga anageuka chui.

Sasa hivi vijana wengi wanapambania kuishi kupitia Umachinga. Miji yote imejaa mabanda nchi nzima.

Ndani ya miaka ijayo hali itakuwa mbaya zaidi ya hii.

CCM wao kazi yao ni kuteuana tu na kutumia majeshi kunyamazisha watu wengine. Walishakata tamaa.

Leo nchi ina watu 60M, lakini inewashinda, itakuwaje miaka 20 ijayo ambapo population itagonga karibu 80M-100M.
 
Inafahamika kwamba ukifaulu vizuri unajiweka sehemu nzuri zaidi.

Vijana wakiwa vyuo lazima msome sio show off tu kila weekend.
Oh yes, well said my friend!!

Aaaaaaa wanafunzi vyuoni siku hizi ni vituko vitupu, wala maadili hakuna Kabisa.

Watoto wa kike wanashindana kuwa na handbags hawataki kushika madaftari mkononi tofauti na enzi zetu.

Kigezo cha GPA ni kizuri sana ili wasome kwa bidii.
 
Huu ujinga ni Tanzania tu, kwa sheria ipi? Ni lini serikali iliwataka wahitimu wakajitolee na malazi na posho ya kujikimu nani aligharamia? Huu upumbavu utengenezeni tu ipo siku mtafurushwa kwa maandamano na riots.
Viajira vyenyewe elfu 9, ambavyo mishahara yake ni laki 5 lakini kelele kibaoooo. Upuuzi tu.
 
Oh yes, well said my friend!!

Aaaaaaa wanafunzi vyuoni siku hizi ni vituko vitupu, wala maadili hakuna Kabisa.

Watoto wa kike wanashindana kuwa na handbags hawataki kushika madaftari mkononi tofauti na enzi zetu.

Kigezo cha GPA ni kizuri sana ili wasome kwa bidii.
Sometimes kusoma sana au kutosoma hakudetermine GPA kubwa.

Huko "Private" vyuo vingi wanapeana miGPA mikubwa mikubwa tu wakati vyuo vingi serikalini wanafunzi wana kazi ya kuoneshana umwamba na ma-lecturerers.
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido Kiruswa aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea. Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo.

Amesema kigezo kikubwa kitakachotumika ni hicho akiongeza kuwa, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka.

========

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.

Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.

Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.

Suara la ajira likichukuliwa kua serikali ndio muajiri mkuu Bado tuna safari ndefu nibora hao wenye vyeti vya ualimu busara wàkachukue kozi nyingine watazidi kuongezeka wakosa ajira nashauli vyuo vya ualimu vibadilishwe vitoe taaluma nyingineya elimu imetosha kwani mwaka kesho watafika wahitimu laki moja wanaenda wapi wanatutosha bila wapya miaka Kumi ijayo kwa kuajiri hata walimu 10.000 kila mwaka ni kubadirisha taaluma vyuo vitoe fani ambazo mhitimu anaweza kuajiliwa au kujiajiri
 
Kwahiyo taaluma gani ambayo haiwezi kuwa saturated ?
 
Alalamikia barua feki? Kwanini kwenye mfumo waliojitolea wasitume recommendations letter ya eneo au shule aliyekuwa anajitolea? Kwanini barua hizo hazikupita kwa Wakurugenzi, madc wa maeneo husika? TSC wapo, TISS wapo, wakaguzi wa shule wapo, maafisa elimu wapo, Ummy mwalimu angalia sasa usiniangushe. Bora ajira zichelewe ila tena haki bin haki.
Mi nadhani wa kusema ukweli kabisa ni kamati za shule ndiyo huwa zinahangaika kuwatunza.
 
Hizo nafas zenyewe za kujitolea hazikuepo ukienda kuomba nafasi ya kujitolea unaambiwa hamna
 
Huwezi kuajiri wote lazima utengeneze criteria ndio maana miaka ya nyuma walimu walikuwa wanaajiriwa automatic kwakuwa nafasi zilikuwa nyingi kwasasa mambo yamebadilika.

Survival for the fittest
Watu wengi wanachapia ety "survival for the fittest" correct statement is "survival of the fittest" na bahati nzuri nipo tamisemi hapa hapa ntaanza na ww kukukata🤣🤣🤣😇😅
 
Alalamikia barua feki? Kwanini kwenye mfumo waliojitolea wasitume recommendations letter ya eneo au shule aliyekuwa anajitolea? Kwanini barua hizo hazikupita kwa Wakurugenzi, madc wa maeneo husika? TSC wapo, TISS wapo, wakaguzi wa shule wapo, maafisa elimu wapo, Ummy mwalimu angalia sasa usiniangushe. Bora ajira zichelewe ila tena haki bin haki.
Unajindanganya na hujawahi kuomba hata nafasi ya usimamizi wa uchaguzi ukajionea upendeleo
 
Waziri ummy mimi nakushauri waagize wakurugenzi,maafisa elimu au wakuu wawilaya wapitie shule zote katika halmashauri zao utapata waalimu sahihi wanaojitolea,maana itakua niuonevu mtu aliejitolea akose na yule ambaye hajajitolea apate. Ushauri mwingine akangalia wale waliokaa mtaani kwa mda mrefu alafu wamejitolew mfano kuna waalimu waliomaliza 2015 wengi ni art diploma na degree hawa hawajaajiriwa wape kipaombele
 
Kwahiyo taaluma gani ambayo haiwezi kuwa saturated ?
Kwa mfano mifugo unaweza kua afisa wa mifugo au mfugaji kiilimo unaweza kua afisa kiilimo au mkulima uvuvi afisa uvuvi au mfuga samaki lakini kwa kua sekta hizo zinaonekana hazina maana lakini ndizo zenye kuweza kubeba watu wengi na Zina mahitaji muhimu kwa bHinadamu tangu bidhaa ya awali mpaka ya mwisho ktk mnyororo wake zikifanyika kitaalamu
 
Maafisa mifugo wako wengi tu mtaani, jobless.
 
Huu ujinga ni Tanzania tu, kwa sheria ipi? Ni lini serikali iliwataka wahitimu wakajitolee na malazi na posho ya kujikimu nani aligharamia? Huu upumbavu utengenezeni tu ipo siku mtafurushwa kwa maandamano na riots.
We waache tu, hapo dawa ni moja... Hao vijana watakaokosa kazi wote waandike barua za kuomba kwenda kujitolea halafu wakinyimwa waandamane kudai haki yao ya kujitolea maana kigezo ni huajiriwi mpaka ujitolee.

Haiwezekani vijana wote kwenda kujitolea tena government pekee, na wanaojitolea private je?
 
Watu wengi wanachapia ety "survival for the fittest" correct statement is "survival of the fittest" na bahati nzuri nipo tamisemi hapa hapa ntaanza na ww kukukata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji56][emoji28]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom