Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Tamko limeshatolewa. Wa kujitolea watapewa kipaumbele. Hii ishu ya GPA kubwa ina walakini. Wengine wana GPA kubwa kwa kupitia njia isiyo rasmi ya kuwafurahisha Wakufunzi wao.
Hiyo ya kujitolea kuna wengine hawawezi, coz maisha hayakidhi yeye kujitolea, waangalie upya hili suala la ajira ktk kuondoa kero kwa waombaji.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Watu wengi wanachapia ety "survival for the fittest" correct statement is "survival of the fittest" na bahati nzuri nipo tamisemi hapa hapa ntaanza na ww kukukata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji56][emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mimi si Mwalimu,lakini nashauri wasiangalie GPA. Wakitaka kuangalia hilo basi itawapasa waanalie na ranking ya vyuo.

Kuna vyuo kupata GPA ya 3.9 siyo issue kubwa ila kuna vyuo kupata tu hiyo 3.0 ni shangwe.
Kuitafuta 3.9 mkwawa ni kuitafuta pepo
 
Watu wengi wanachapia ety "survival for the fittest" correct statement is "survival of the fittest" na bahati nzuri nipo tamisemi hapa hapa ntaanza na ww kukukata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji56][emoji28]
Hahahaha wewe 47 mimi sio Mwalimu bhana.Hapo kwenye survival kweli nimechapia kiuandishi.
 
Ninashauri, walioomba na wakakosa ni vema wakajibiwa kwamba wamekosa na wakapewa sababu za kukosa, waliopata vile vile wajibiwe kuwa wamepata na sababu za kupata kuliko ukimya uliopo, unafanya mamilioni ya watafuta kazi kulalamika mitaani.

Pili, mfumo huo uangalie gender pia, kuna uwezekano kuajiriwa gender moja tu. Kwa ujumla mfumo wa ajira uangalie mikoa, wilaya, dini, umri, ufaulu, wenye mikopo, yatima, uwezo wa kifamilia, masomo yenye manufaa kwa sasa, ulemavu, uraia, nk.
kaka Ajira hazizwezi kutolewa kwa kufanya ubaguzi wa hivo vigezo ulivyoweka, aliyekidhi vigezo vilivyowekwa kwa kiasi kikubwa kuliko wengine anapaswa kupata bila kuangaliaa jinsia yake, dini , hali yake ya kiuchumi n.k.
 
Habari ya kuajiriwa waliojitolea tu sio nzuri kabisa. Yani ajira hakuna halafu mtu uende ukajitolee badala ya kutafuta njia nyingine mbadala ya kutoka kama kujiajiri na kwenda kujitolea nje ya fani yako. Kama hao 89,000 wote wangejitolea je wangetosha kwenye vituo? Serikali wawe na kigezo bora cha kuajiri na sio chenye upendeleo au ubaguzi wa aina hii. Hii sio fair kabisa.

Kutosha wangetosha ila tatizo ni wangeishijee? Maana hapo kuna watu wana miaka 5 mtaani
 
Mwendazake alisema wanatengeneza ajira milioni 9! Yan Walikuwa kama majuha! Elfu 6 tu inawashinda
 
Na kuna wana watafoji waonekane walijitolea na huku hawajawahi kujitolea kabisa
 
Waziri ummy mimi nakushauri waagize wakurugenzi,maafisa elimu au wakuu wawilaya wapitie shule zote katika halmashauri zao utapata waalimu sahihi wanaojitolea,maana itakua niuonevu mtu aliejitolea akose na yule ambaye hajajitolea apate. Ushauri mwingine akangalia wale waliokaa mtaani kwa mda mrefu alafu wamejitolew mfano kuna waalimu waliomaliza 2015 wengi ni art diploma na degree hawa hawajaajiriwa wape kipaombele
Na hafanyi unachotaka tuone sasa
 
Ili kujua hii nchi ya kijinga:
Unaongeza siku za kutuma maombi wakati nafasi ni 70000 na tayari waliokwoshatuma ni zaidi ya Laki.
 
Wengi humu wanaangalia solution ya muda mfupi, wakati bado vyuo vinatema.

Hili tatizo limetengenezwa na hao Wizara ya elimu na TCU yao.

Mtu anaenda kusoma education kwasababu
1. Apate mkopo
2. Programme nyingine zimemtema ualimu ndio kapu la kubeba walioshindwa kwenda labda health programmes.

Lazima watu wajazane wawe wengi sanaa kwenye hiyo fani na wakose pakwenda.

Nashauri
1. TCU iweke vigezo vikali kwenye programmes za ualimu tupate walimu kweli, wenye kupenda ualimu na sio igeuke ni kimbilio la mwisho kwa wanaojiunga na elimu ya juu.
Hii iende sambamba na kuboresha maslahi ya walimu iwe taaluma inayoheshimika.
 
Maafisa mifugo wako wengi tu mtaani, jobless.
Kama wako mitaani naHawajishughulishi na ufugaji wowote watambulike na wasipate kabisa ajira kwani wamesha onesha kua hawana taaluma hiyo hivyo hawatakua na ushauli wowote katika nausea ya mifugo
 
Kama wako mitaani naHawajishughulishi na ufugaji wowote watambulike na wasipate kabisa ajira kwani wamesha onesha kua hawana taaluma hiyo hivyo hawatakua na ushauli wowote katika nausea ya mifugo
Hawatakua na tija katika sekta ya mifugo
 
Huu ujinga ni Tanzania tu, kwa sheria ipi? Ni lini serikali iliwataka wahitimu wakajitolee na malazi na posho ya kujikimu nani aligharamia? Huu upumbavu utengenezeni tu ipo siku mtafurushwa kwa maandamano na riots.
wewe ndiye huelewi- duniani kuna internship
internship



noun

the position of a student or trainee who works in an organization, sometimes without pay, in order to gain work experience or satisfy requirements for a qualification.

"they encouraged students to apply for newspaper internships"
 
Back
Top Bottom