Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu ameahidi kufanya mabadiliko makubwa kwa watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya watumishi na Wakuu wa Idara katika mamlaka hizo.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika utumishi wa umma, ambapo amebainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakitengeneza madaraja kati yao na watumishi wanaowasimamia.
Aidha, Mhe. Ummy amesema ofisi yake inakusudia kufanya mabadiliko ya utaratibu wa watumishi na watendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo kuondoa mamlaka za nidhamu kutoka kwenye Baraza la Madiwani.
Chanzo: ITV