Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri wa afya mh Ummy muda huu anazungumza na viongozi mbalimbali wa dini juu ya mikakati ya kudhibiti Corona.

Kwa sasa anaongea Shehe wa mkoa wa Dsm slhad Mussa Salumu ambaye anawalaumu baadhi ya viongozi wenzake wa dini wanaoshindwa kutekeleza maagizo ya wizara.
Walikua wapi wasizuie imported cases? Kwanini walikua wanaruhusu watu waingie kutoka kwenye nchi zenye huu ugonjwa?

Ndio madhara ya kuchagua wajinga watuongoze.

Huu ni upuuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile wiki mbili nadhani sasa zinaelekea kutimia,huu ndo wakati hasa wa ku apply safe distance na kuosha mikono.

Nimegundua kwenye uoshaji mikono wahudumu mfano wa maduka, bar etc hawaoshi mikono kabla na baada ya kumuhudumia mteja mmoja.

Wakati wait ndo wanakamata pesa kutoka kila mtu, hii Ni hatari maana mfano uko bar,umeagiza beer,umenawa, muhudumu kakufungulia bia,kumbe mikono yake imeshika pesa za mtu mwingine na iko taitend, anaacha virusi kwenye chupa,wewe unakamata chupa unakunywa huku unaperusi mtandaoni, bila kujua umeshika virus na umehamishia kwenye simu.

Unamaliza bia unalipa,unanawa na kuondoka huku ukiperusi,umesahau Sasa simu Ina virus,unapeleka virus kwako,unaingia ndani unashika kitasa cha mlango, umeacha virus.

Unashika chupa ya chai,umeacha virus,hivyo yeyote atakaeshika hizo sehemu anaingia kwenye mlolongo
 
Atakapoanza kuugua waziri ndio mtajua hii sio movie ya kibongo
Mmejawa na kiburi na uongo mwingi kwa sababu ya mtu mmoja hivi

Ummy sijui utawaambia nini WaTz tukianza kwanza tumeanza kuzikana
Covid-19 Tz ipo kila mahali

Mnaleta siasa kwenye uhai wa watu
Uzuri huyu virus hana uchaguzi ni wote kwa wote
Wakusanya watu akina bashite na wengineo muanze kujiandaa

Punguzeni viburi
 
Kama Mh. Mwalimu waziri wa Afya alivyosema maambukizi yamehamia kuwa ya ndani, ninamshauri na kumuomba Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliangalie suala la mikusanyiko ya nyumba za Ibada kwa mapana.

Kiukweli nyumba za Ibada zinapaswa kuacha kuendelea kukusanya waumini ikizingatiwa mikusanyiko ni moja ya njia za kuongeza maambukizi kwa umma. Ushauri wangu mikusanyiko ya nyumba za Ibada izuiwe. Mh. Rais unaweza kuwaita viongozi wa Imani tofauti na kuwaeleza hili kabla hali haijawa mbaya!
 
Wacha tufe! Binadamu tumekuwa wengi sana kwenye uso wa Dunia! Hivi sasa tunakaribia watu Bilioni nane huku binadamu ambao wamesha kufa mpaka sasa tangu kuumbwa kwa Ulimwengu wakikadiriwa kuwa Bilioni 50! (Hii ni zaidi ya miaka 5000 BC na miaka mingine 2000 AD wamekufwa watu bilioni 50)!

Kwa maana hiyo Annual rate of death has been somewhere around watu milioni 7. (50,000,000,000/7000).
Korona haijaweza kuua hata watu laki tano kati ya watu milioni saba 'wanaotakiwa kuwa wamekufa' kwa mwaka Duniani!
 
Haya yote ni upuuzi wa wanaotuongoza. Tangu kauli ya Rais ya kuwataka watu wa dini wasiache mikusanyiko ya ibada na siasa zilivyofuata nikajua kuna mawili.

Tukipita salama Rais atafanyiwa sherehe ya kumpongeza kwa kauli zake tata kuhusu hatua za kufuata. Na kufikia malengo ya sherehe kwake ndio huo mlolongo wa takwimu zinazowekewa mashaka.

Pili ikitokea mambo yamekwenda kinyume kama inavyotarajiwa hapa nguvu itatumika kwa wakosoaji na usishangae watu watakwenda jela na hata kupoteza maisha vile tu wakikosoa hatua za awali za mheshimiwa wa maweni.

Uhai wetu wanauchezea kamali ila tu wafahamu wao ndio wenye mdororoo mkubwa afya kulinganisha na sisi joggers, kisa cha waziri wa uingereza kitoshe kuwafunza hakuna aliye salama mbele ya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaogoopa mtafikiri mlikuja ishi milele? Kufa kufa tu, si Corona, malalia ajali n.k, Vyote ni namna ya kufa tu

Tustishane bhana! Corona ndo Nani Mbele ya aliyetuumba? Anayei ijua Kesho Yetu yeye ndo awe msemaji wa mwisho,

Cha msingi, Zingatia maelekezo ya wataalamu na mtu akiwa na daliri za Corona ni Bora kujitenga mbali na wengine pia familia yako

Serikali yetu iko kazini masaa yote, tunawapongeza viongozi wetu Kwa kuendelea kutupa tarifa na kitelimisha, Barikiwa Mh Ummy
 
Back
Top Bottom