Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Asante Waziri kwa jitihada zako za kuhakikisha sekta ya afya inawajibika ipasavyo kwa wananchi.

Lakini naona kama unazunguka sana kuhusu kutatua tatizo la uhaba wa dawa mahospitalini.

Wiki iliyopita hapa JF tulitoa maelezo kwa kifupi kuhusu sababu za uhaba wa dawa kwamba ni kwasababu ya Uongozi mbovu wa MSD.

Achana na kukimbizana na hayo maduka ya dawa yaliyokaribu na hospitali maana haitakusaidia kitu kwanza dawa zenyewe hakuna. Fuatilia kilichoandikwa humu JF na ndo mwarobaini wenyewe.


Halafu inaonekana kama vile vionvozi wa hii Serikali mnaogopa kuuwajibisha uongozi wa MSD, mmekuwa mkiyalea matatizo pale Bohari ya Dawa tangu wakati wa Dorothy. Leo tena nimemsikia PM Majaliwa akiwa Manyara akiibembeleza MSD kuhusu kupeleka dawa Manyara, hivi MSD wanatakiwa wafanye kazi kama zimamoto kila wakati wakati hiyo ndo kazi yako?

Pelekeni nguvu zote MSD ili dawa zinunuliwe maana Serikali ya Mama Samia ilishaleta hela kibao hapa MSD.
 
Serikali iwadhibiti watumishi wake wasiibe kama ni kweli wanaiba,Ihakikishe uwepo wa dawa Aina zote katika vituo vyake vya kutolea huduma,jambo ambalo ni gumu Sana,Kwa sababu daktari huandika dawa Kwa mtazamo wake na sio kuangalia kilichopo pharmacy ya Kituo.
Mwizi wa hizo dawa anaweza kuiba mkoa X na kwenda kuuza mkoa y.Hivyo Hilo tamko na hiyo Sheria kama Ipo haina tija.Ni maamuzi ya kihisia zaidi.
 
Wizara imepata chiriku, Kila wiki ni matamko na makatazo na mikwara ya kufa mtu,

Huyu mmama anapenda kuongea ongea sana, kila analoliwaza yeye anataka aliongee
Na kwanini hyo maduka yabanane kaibu na hospitali? Waziri yuko sahihi sana, Ummy ni miongoni mwa mawaziri jembe nchi hakuna asiyemfahamu. We inaonekana umeguswa. Hamna hata ubinadamu mnavizia kuwaibia wagonjwa wakati na nyie ni wagonjwa watarajiwa. Oneni hata aibu.
 
Yaani sababu hasa ni nini?..weka na sababu, mfano mimi nina frame zimepakana na hospitali na wamefungua pharmacy, sasa watakuja kuondoa hiyo pharmacy na kodi nani atamrudishia?
ndiyo sheria imeshatungwa utajuana na mwenye nyumba. Kutokujua sheria haikuoatii udhuru.
 
Km hujaelewa sidhani km utakuja kuelewa. Umeambiwa watumishi wa Hospitali wasio waaminifu wanakula njama na wenye maduka ya dawa kwa kuuziwa madawa ya serikali na ndio sababu mojawapo inayofanya hospitali nyingi za serikali kuishiwa dawa mapema.
 
Pale akili ndogo zinapotawala akili kubwa...Aisee...sijaelewa lengo la huyu Mama eti waziri ni lipi hapa? Kwani wakipeleka hata mita 1,000 dawa zitapatikana Hospitali au itakuwa ndio mbaya zaidi kwa wagonjwa kutembea hayo makilomita kutafuta dawa? mwizi ni mwizi tu na dawa yake ni kumzuia asiibe na sio vinginevyo..
 
Simple logic wao wameshindwa nini kuhakikisha dawa zinapatikana hospitali muda wote ili watu wasiende maduka ya nje?

That's hasty generalization.
 
Karibu na hosp ndio wateja wao walipo ni sawa na uulize mbona stand za mabasi kuna vyoo vya kulipia
 
Anaongea ili mradi tu naye aonekane ameongea .naona amepanic yeye amepeleka kiasi gani msd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye anajali nini bana mshahar 11m posho ya mafuta umeme bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahitaji ya hospital ni makubwa mno sasa wanaletewa vimilioni viwili ndo wanakuja kusingizia wizi wa dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu wanategemea na kodi ije kuwalipia mafuta ya v8 na allowance kibao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…