Waziri Ummy Mwalimu suala la Uhamisho kwa Watumishi wa umma litatue

Waziri Ummy Mwalimu suala la Uhamisho kwa Watumishi wa umma litatue

Pilitoni

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
1,197
Reaction score
507
Binafsi nikupongeze kwa kuteuliwa kuwa Waziri katika OR- TAMISEMI, wizara hii ni kubwa na ina changamoto nyingi.

Wizara hii utaiweza tu pale utakaposhirikiana vyema na wenzako na pia kuwa tayari kupokea na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoibuliwa na siye wananchi tulioko mashinani, mkipuuzia shauri yenu mtakumbuka siku moja.

Lengo hasa la bandiko hili nikukuomba ndugu Ummy Mwalimu uweze kuingilia kati suala la Uhamisho kwa Watumishi wa umma walioko chini ya TAMISEMI, kuna wengine walikamilisha taratibu za uhamisho miaka miwili iliyopita lakini mpaka leo OR-Tamisemi hawajatoa vibali, ukiulizia huko unajibiwa uhamisho umesitushwa.

Hawa watu wengine ni wagonjwa wanahama kusogea karibu na huduma za afya mbona mnawatesa hivi?Niseme tu Waziri aliyepita Jaffo alikuwa hajali kabisa kwenye media ni machachari kwelikweli na matamko kibao, ukiwasilisha kero kwake hata hashughulikii,hiyo tabia siyo nzuri.

Ukiwa Waziri tatua kero za watu na siyo lazima uonekane kwenye maTv ukifoka, mazuri yako watu watayasema tu hata kama hujaonekana kwenye public,huko alikopelekwa ajirekebishe.

Waziri Ummy, hili suala la Uhamisho naomba sana ulitatue linasumbua sana wafanyakazi, inafikia kipindi hadi watumishi wanatoa rushwa hapo ofisini kwako ili wapatiwe vibali vya uhamisho, hiyo njia haikubaliki hata kidogo.

Mtumishi kaomba uhamisho yeye mwenyewe kwa sababu za msingi kabisa, anajihamisha yeye mwenyewe kwa matatizo yake na wala Serikali haimlipi chochote na anapokwenda ni ndani ya Tanzania hii hii kwenda kuwatumikia Watanzania wengine halafu anazuiliwa na ananyimwa kibali.

Hilo Waziri Ummy ni lako, lione na kisha ulitatue.

Mungu ibariki Afrika.

Mungu ibariki Tanzania na

Mungu Wabariki Watanzania wote.

Ahsanteni Sana.
 
Mh. Ummy ni Msikivu sana, ninatumaini atafanyia kazi Changamoto nyingi za Wizara ya TAMISEMI.
 
Back
Top Bottom