JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mdau kwenye mtandao wa Twitter ametoa hoja yake kuhusu bima na kuwatag Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Viongozi wa Taasisi ya NHIF na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima.
Ameandika: “Kilio cha Wazazi wengi kwa Sasa ni Swala la Ku Apply Bima ya Afya kwa watoto kisha ikae Miezi 3 ndio waweze Kuitumia halijakaa sawa. Tunaomba mpitie Kipengele hiki cha muda wa Kusubiri Mkirekebishe.
Waziri Ummy Mwalimu akajibu: “Tatizo baadhi ya watu wanakata Bima ya Afya tayari wakiwa ni wagonjwa tena wengine wakiwa wodini. Hatua hii inatishia uhai na ustahamilivu wa Mfuko. Nitumie fursa hii kuhimiza wananchi kukata Bima ya Afya kabla ya kuugua.”