Inawezekana umesomea mambo hayo lakini umekariri vibaya. Yes, Waziri maybe anazungumzia issue ya "adverse selection" lakini majibu aliyotoa ni tofauti na hoja ya aliyejibiwa.
Miongoni mwa matatizo ya wasomi wetu ni kutotumia usomi kwenye kutekeleza majukumu yao. Ndio maana kuna uzi wa
johnthebaptist anasema kuna kazi zinazofanywa na baadhi ya taasisi zinaweza kufanywa na lasaba B.
Tatizo lingine la wasomi wetu ni kutokuwa na uwezo wa kutambua kiini cha tatizo na suluhu yake na hili ni tatizo la kutoelewa dhana ya vitu kuhusiana na kusababishana (ignorance about correlation and causation). Matokeo yake decision zinazofanywa zimekuwa zikiumiza kundi kubwa la watu ambao hawahusiki.
Tatizo la tatu ni kutoelewa "operational models za taasisi au mambo mbalimbali na madhara yake au mabadiliko yake. Mfumo wa Bima ya Afya nadhani ni lazma kwa mtumishi wa umma (kama sijakosea), no matter kama mtumishi huyo na wanufaika wake wanajijua kama wana historia ya kuumwa umwa au hapana. Na kutokana na hilo NHIF imekuwa Taasisi hodhi ya Bima ya Afya nchini kwetu. Hii ni kutokana na kuangalia upande mmoja tu wa kupata pesa kutoka katika mapato ya mtumishi.
Kwa maoni yangu, huenda tatizo hilo lingeisha kama watumishi pamoja na ulazima wa kuwa na Bima ya Afya, lakini wangepewa chaguo la kujiunga na Bima ya Afya waitakayo. Kwa kufanya hivyo, tatizo analosema Waziri huenda lisiwepo au likapungua kwani mfuko wenye ushindani dhaifu ungeondoka sokoni na pia historia ya mgonjwa ingetumika katika kutambua package inayomfaa. Changamoto za afya zimeongezeka kutokana na kuongezeka kwa presha ya maisha, na pia idadi ya watumishi wa umma imekuwa ikiongezeka kwa kasi kiasi cha NHIF kuzidiwa.
Aidha, kutowaadhibu wasiohusika, kungekuwa na mfumo wa matibabu uliounganishwa (integrated health services, IHS) ambapo historia ya mgonjwa inaweza kuonekana wakati wowote na popote anapoenda kupata huduma za afya (na hivyo kupunguza athari za kuficha maradhi wakati wa kukata bima).