Waziri Ummy punguza kujieleza, unajifunga sana katika maelezo yako

Waziri Ummy punguza kujieleza, unajifunga sana katika maelezo yako

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Dada Ummy sina shaka na utendaji kazi wako lakini nakushauri upunguze kujieleza kwa sababu maelezo unayotoa yanakufunga.

Mtangulizi wako pamoja na kuwa na maneno mengi lilipokuwa linakuja suala nyeti la kitaifa alikuwa makini sana kuchunga kauli zake ili kuepusha maswali na mijadala isiyo ya lazima kwa watu.

Unachotakiwa utambue ni kuwa wizara uliyopewa ina changamoto nyingi kwakuwa inagusa karibia kila sekta kuanzia afya, elimu, miundombinu, wafanya biashara pamoja na ajira kwa vijana.

Kwahiyo ni wizara inayohitaji umakini na utulivu mkubwa kuiongoza kabla ya kuamua au kutamka jambo lolote unalotaka umma usikie vinginevyo utakuwa unajifunga kwa kauli zako kila wakati.

Mathalani nitolee mfano suala hili la ajira. Hapakuwepo haja ya kutaja idadi ya waombaji ikiwa bado maombi yanaendelea kwa sababu umeleta tension kubwa na hali ya kukata tamaa kwa waombaji.

Kadhalika suala la vigezo vya kuajiri lingebaki kuwa siri yenu wizarani ili waombaji wabaki na kazi moja tu ya kusubiria majina au pdf kama wengi wanavyopendelea kuita. Lakini kusema wizara inafikiria kutumia kigezo hiki na kile unazidi kuwajengea hofu waombaji na kujifunga pia endapo mambo yatakwenda tofauti na ulichokisema.

Nikupe mfano mwingine. Ukiwa bungeni leo umesema wizara itatoa kipaumbele kwa wahitimu wa miaka ya 2012 lakini kumbu kumbu zinaonyesha wahusika hao walishaajiriwa na hawapo. Katika kuthibitisha hili nimekuwekea viambatanisho vya matangazo ya ajira 2019 na 2020 ambayo yote yanaonyesha wahitimu waliopo ni kati ya 2014 na kuendelea..

Kiambatanisho 1: Tangazo la ajira za mwaka juzi likionyesha wahitimu wa kuanzia 2014-2017

IMG_20210525_0001.jpeg

Kiambatanisho 2: Tangazo la ajira la mwaka jana likionyesha wahitimu waliopo ni kuanzia 2014-2019
IMG_20210525_0002.jpeg

Lakini tangazo lako linasema kuna wahitimu hadi wa 2012 na 2013 na wewe mwenyewe umekiri kwamba mnafikiria kutoa priority kwa wahitimu hao ambao takwimu zinaonyesha tayari walishaajiriwa miaka ya nyuma huko pamoja na wahitimu wa 2014. Je, inakuaje tena uwape kipaumbele wahitimu hawa ambao serikali iliwaajiri miaka kadhaa iliyopita?? Kama waliacha kazi kwa hiari zao unahangaika nao wa nini dada ummy??
 
Mara nyingi ukimuona mtu yeyote anazungumza sana,ujue hana umakini Na hicho anachokielezea! Mtu akikijua kitu kwa umakini anakuwa hana maneno mengi! Anakuwa very precise!!
Umenena kitu cha msingi sana. Ummy angepunguza kuwa mwongeaji maana watu wakimsoma hulka yake ni rahisi sana kuyumbishwa ni kama mwendazake alivyokuwa anapenda kusifiwa akiamini wote wanaomsifia wanampenda kumbe wengine walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kusudi watimize malengo yao.
 
Mdomo uliponza kichwa.

Mtego wa binadamu kwa binadamu mwenzake wala shimo halihusiki. Isipokuwa ukijichanganya tu.
Ulichokisema ni sahihi kwa sababu asili ya watanzania ilivyo unaweza kuongea sana wakabaki wanakusikiliza na kukutazama tu lakini ukijichanganya kidogo wanaitumia weakness hiyo kukuharibia hata kama kutakuwa na mazuri kiasi gani uliyotenda. Ummy awe makini sana.
 
Umenena kitu cha msingi sana. Ummy angepunguza kuwa mwongeaji maana watu wakimsoma hulka yake ni rahisi sana kuyumbishwa ni kama mwendazake alivyokuwa anapenda kusifiwa akiamini wote wanaomsifia wanampenda kumbe wengine walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kusudi watimize malengo yao
Mkuu mbona unamsema Ndugai
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa sasa ni vema ukafanya mabadiliko ya viongozi wa wizara mapema kabla ya mambo kuharibika kabisa..heri shari kuliko shari kamili.

Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu ameshindwa kuiongoza TAMISEMI

Hii wizara imekuwa kubwa kulingana na uwezo wake, Rais unatakiwa umtoe mapema iwezekanavyo

Waziri huyu amezua taharuki ya ajira kwa watanzania, kwa jambo kama hili tu huyu anatia shaka kama anaweza simamia mapato ya halmashauri kisawasawa.

Rais tunaomba utuondolee huyu mtu, kama hakuna mwingine ni vema Jaffo arudishwe!
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa sasa ni vema ukafanya mabadiliko ya viongozi wa wizara mapema kabla ya mambo kuharibika kabisa..heri shari kuliko shari kamili.

Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu ameshindwa kuiongoza TAMISEMI

Hii wizara imekuwa kubwa kulingana na uwezo wake, Rais unatakiwa umtoe mapema iwezekanavyo

Waziri huyu amezua taharuki ya ajira kwa watanzania, kwa jambo kama hili tu huyu anatia shaka kama anaweza simamia mapato ya halmashauri kisawasawa.

Rais tunaomba utuondolee huyu mtu, kama hakuna mwingine ni vema Jaffo arudishwe!
Leo hii ndiyo mnajifanya wakosoaji wa uongozi wa mama Samia wakati awamu ya jiwe mlikuwa mabubu
 
Utakuwa jafo gang wewe. Jaffo ndiye alikuwa mbovu zaidi na nyungu zake
 
2012-2014 walibaki wale waliopangiwa kazi vijijini wakagoma kwenda
 
TAMISEMI ni wizara iliyolundikiwa idara nyingi ndo maana haitawezekana kuwa na ufanisi, hakuna waziri aliewahi kuimudu wizara hiyo badala yake imekuwa wizara yenye madudu kibao kuliko wizara yoyote hapa nchini, dawa yani kupunguza idara nyingine ziende wizara mama, mfano elimu na afya
 
Huwez kufananisha jafo na ummy ,ummy yupo vizuri zaidi mfano jafo alisema ameajiri waaalimu 13000 kumbe zilikua alfu nane ,badae ndio wakasema wataajiri hizo elfu tano zilizobaki,
 
Da Ummy is good kwa wizara kama sheria na katiba. Ila TAMISEMI au AFYA au any "complex" ministry ni ngumu sana kwake kuleta impact. Ana vijimaneno maneno viingi vile vya kwetu. Dorothy pamoja na vituko vyake vingi, would effectively manage this ministry. Maana anaweza kumkaba mtu na kumtapisha pesa ya umma aliyokula. Ummy no. I repeat again, she is very lightweight. Kulalamika tuuuu. Mara utamsikia anasema DED jipime kabla mama hajakuondoa!!!. Hizi ni kauli za weak people.
 
Na kuhamasisha waombaji wakatafut barua za kujitoea hata kwa kuonga au kughushi
akini kusema wizara inafikiria kutumia kigezo hiki na kile unazidi kuwajengea hofu waombaji na kujifunga pia endapo mambo yatakwenda tofauti na ulichokisema
 
Back
Top Bottom