Waziri Ummy punguza kujieleza, unajifunga sana katika maelezo yako

Kumtaka ( Kummwambia ) Mtu wa Tanga apunguze ( aache ) Kujieleza tena kwa kutoa ' Pumba ' nyingi kama Waziri Ummy Mwalimu ni kupoteza tu muda wako.

Rudi katika Medani za Michezo mtizame Afisa Mhamasishaji wa Yanga SC Antonio Nugaz ambavyo huwa ' anabwabwaja ' hovyo tu akihojiwa na huwa hana la maana.

Tunu ya Watu wa Tanga ni Porojo sana.
 
Huwez kufananisha jafo na ummy ,ummy yupo vizuri zaidi mfano jafo alisema ameajiri waaalimu 13000 kumbe zilikua alfu nane ,badae ndio wakasema wataajiri hizo elfu tano zilizobaki,
Sipingi hoja yako ndio maana kwenye post yangu nimeanza kwa ku declare interest kukubali utendaji kazi wake ila ninachopinga ama kushauri ni kumtaka apunguze kujieleza na kuongea sana kutamuharibia
 
Dada Ummy sina shaka na utendaji kazi wako lakini nakushauri upunguze kujieleza kwa sababu maelezo unayotoa yanakufunga.

Mtangulizi wako pamoja na kuwa na maneno mengi lilipokuwa linakuja suala nyeti la kitaifa alikuwa makini sana kuchunga kauli zake ili kuepusha maswali na mijadala isiyo ya lazima kwa watu.

Unachotakiwa utambue ni kuwa wizara uliyopewa ina changamoto nyingi kwakuwa inagusa karibia kila sekta kuanzia afya, elimu, miundombinu, wafanya biashara pamoja na ajira kwa vijana.

Kwahiyo ni wizara inayohitaji umakini na utulivu mkubwa kuiongoza kabla ya kuamua au kutamka jambo lolote unalotaka umma usikie vinginevyo utakuwa unajifunga kwa kauli zako kila wakati.

Mathalani nitolee mfano suala hili la ajira. Hapakuwepo haja ya kutaja idadi ya waombaji ikiwa bado maombi yanaendelea kwa sababu umeleta tension kubwa na hali ya kukata tamaa kwa waombaji.

Kadhalika suala la vigezo vya kuajiri lingebaki kuwa siri yenu wizarani ili waombaji wabaki na kazi moja tu ya kusubiria majina au pdf kama wengi wanavyopendelea kuita. Lakini kusema wizara inafikiria kutumia kigezo hiki na kile unazidi kuwajengea hofu waombaji na kujifunga pia endapo mambo yatakwenda tofauti na ulichokisema.

Nikupe mfano mwingine. Ukiwa bungeni leo umesema wizara itatoa kipaumbele kwa wahitimu wa miaka ya 2012 lakini kumbu kumbu zinaonyesha wahusika hao walishaajiriwa na hawapo. Katika kuthibitisha hili nimekuwekea viambatanisho vya matangazo ya ajira 2019 na 2020 ambayo yote yanaonyesha wahitimu waliopo ni kati ya 2014 na kuendelea..

Kiambatanisho 1: Tangazo la ajira za mwaka juzi likionyesha wahitimu wa kuanzia 2014-2017

View attachment 1797443
Kiambatanisho 2: Tangazo la ajira la mwaka jana likionyesha wahitimu waliopo ni kuanzia 2014-2019
View attachment 1797445
Lakini tangazo lako linasema kuna wahitimu hadi wa 2012 na 2013 na wewe mwenyewe umekiri kwamba mnafikiria kutoa priority kwa wahitimu hao ambao takwimu zinaonyesha tayari walishaajiriwa miaka ya nyuma huko pamoja na wahitimu wa 2014. Je, inakuaje tena uwape kipaumbele wahitimu hawa ambao serikali iliwaajiri miaka kadhaa iliyopita?? Kama waliacha kazi kwa hiari zao unahangaika nao wa nini dada ummy??

Ukiona mtu anajichanganya katika maelezo ujue kazi hiyo haiko kwenye damu yake ni kama anasukumwa kufanya alimradi liende, akikujibu hayo maswali kiufasaha njoo kwangu nikupe bata mmoja
 
Amezoea kudanganya huyu binti akisaidiwa na dikteta aliweza kuudanganya ulimwengu wote kuwa hakuna corona Tanzania.
 
Back
Top Bottom