Waziri Ummy: Serikali haitoi taarifa za COVID-19 kutokana na zoezi la uhakiki wa maabara ya Taifa

Waziri Ummy: Serikali haitoi taarifa za COVID-19 kutokana na zoezi la uhakiki wa maabara ya Taifa

Katikati ya vita, unamsimamisha kazi kamanda mkuu wa jeshi - unamwambia akae chini na mwingine achukue injini. .. wakati wote huo wa kufanya hii restructuring je adui yako atakuachia nafasi ujipange kwanza ili ukiwa tayari muanze vita tena?

Tanzania VS Covid -19

Dk ni ya 30 ya mchezo, Tanzania kashafanya Sub mbili, CoVID bado kakomaa... wacha tuone.

(Stay Home)
Well said and well written
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema sababu ya kutotangaza mwenendo wa ugonjwa wa Corona ni kutokana na maboresho yanayofanyika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ambapo kuna marekebisho yanafanyika na ndani ya siku chache marekebisho yatakamilika na watatoa taarifa

Waziri Ummy ameeleza hayo leo wakati akizindua mfumo wa mawasiliano wa huduma kwa wateja katika Wizara hiyo ambapo amesema itasaidia wananchi kupata taarifa sahihi kwa haraka zaidi.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza kuwa vifo vinavyotokana na Corona vipo na kesi za maambukizi zipo, hivyo wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari ili kuepuka kuambukizwa huku akiwataka kufuata taarifa sahihi na kuacha kujawa na hofu.

Chakula ya mwenyekiti imeongea
 
Tanzania kuna mashine moja tu yenye uwezo kupima sampuli ya virusi vya Corona, ajabu ni kwamba Zanzibar wameendelea kutoa takwimu za maambukizi wakati Tanganyika wao wamesimamisha mchakato wa kutoa takwimu kwa maelezo ya kufanyia maboresho ya taarifa za matokeo ya upimaji wakati mashine inayotumika kwa Tanganyika na Zanzibar ni hiyo hiyo moja!
 
Hakuna mwandishi wa habari mwenye uwezo wa kuuliza, Jiulize kwa nini Zanzibar wametoa taarifa wakati bado wanatumia maabara hii hii ambayo inafanyiwa uchunguzi ?
ni mamlaka mbili tofauti ndio maana kule mwenye mamlaka ya kutangaza ni waziri wao na sio ummy.
 
Nikiona neno "uhakiki" napata ukakasi,walisema hawatoi ajira wala kupandisha majalada mpaka wamalize uhakiki,wale wenzangu na mimi hali huko niaje?
 
Dunia hii kupitia historia inatupa fundisho la maana sana, michakato mibovu ya teuzi inawaleta watu wa aina fulani ktk madaraka ili watu wengi wapate kujifunza kupitia makosa yao. Hii hutokana na kutojali ama kupuuzia kwa mambo ya msingi yenye kuhitaji hekima na busara nyingi.

Hapi ndipo ndiyo "weak link" hasa ktk mataifa ya Afrika, na ndipo hutokea makosa ya kuwapa watu nguvu kubwa za kikatiba, kitu ambacho huishia kuwarudi watu wao wenyewe kupitia maumivu yatokanayo na matumizi mabovu ya madaraka ambayo kwa hiari yao wenyewe waliamua kuyakabidhi kwa watu dhalimu na wababaishaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hizo taarifa za idadi ya wafu na wenye corona zinasaidia nini?

Wagonjwa 20, kesho wagonjwa 50, kesho kutwa wagonjwa 100... SO WHAT?

Watu wameshaelekezwa kuchukua tahadhari. Hiyo inatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Zinasaidia ku monitor mwenendo wa maambukizi ili serikal ijue wapi pa kutilia mkazo.
Progress lazima ijulikane. Zingekuwa hazina umuhi sidhani kama nchi zingine wangetaja? Serikal zingekaa kimya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar bwana kumbe wao test kit zao zinafanya kazi..

Naona 5H1 imefuata mzigo Madagascar..

sample..!!
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema sababu ya kutotangaza mwenendo wa ugonjwa wa Corona ni kutokana na maboresho yanayofanyika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ambapo kuna marekebisho yanafanyika na ndani ya siku chache marekebisho yatakamilika na watatoa taarifa

Waziri Ummy ameeleza hayo leo wakati akizindua mfumo wa mawasiliano wa huduma kwa wateja katika Wizara hiyo ambapo amesema itasaidia wananchi kupata taarifa sahihi kwa haraka zaidi.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza kuwa vifo vinavyotokana na Corona vipo na kesi za maambukizi zipo, hivyo wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari ili kuepuka kuambukizwa huku akiwataka kufuata taarifa sahihi na kuacha kujawa na hofu.

Nzuri hii,na Jambo la kushukuru mungu dawa inakuja na pipa RAI yangu kwa wananchi tunywe dawa kwa mwitikio wa nguvu!!!!VIVA MAGUFULI .Leo naiyona COVI19 kuondoka Tanzania . BAVICHA ENDELENI KUSHUPAZA SHINGO ZENU ZITAKATIKA VIPANDEVIPANDE

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Uhakiki upi tena. Kwani before kabla maabara haijaanza kupima haukufanyika uhakiki ?Waandishi kwa nini hamjamuuliza ?
Kaka kwani sikuhizi kuna waandishi wa habari au wachumia tumbo...Press zoote hasa za serikali huwa ni vituko saana siku hizi. Kwa mfano hapo angeulizwa swali rahisi kuwa je kwa Serikali kutotoa majibu ya watu walokwishapima mpaka sasa haoni kuwa wanachangia maambukizi zaidi tena kwa kasi mtaani manake, mtu kama ameenda kupima akaambiwa aende tu nyumbani asubiri majibu (zaidi ya wiki sasa) nini matarajio yao"? Swali la pili hizi mashine zimekuwa "imported" na kuhakikiwa na WHO kabla hazijaanza kutumiwa katika nchi zoote .Haina shaka kwamba sisi uwezo wa wataalamu wetu unaishia katika kupima na kutoa majibu kama walivyovufundshwa sasa je kwa zoezi linaloendelea sasa je wanawashirikisiha WHO au ni zoezi gani linaloendelea tusilolifahamu?!. Nafahamu vyombo vingi vya habari vimewekwa mfukoni awamu hii lakini hata wale wachache waliobaki wenye akili mbona hatuoni mnauliza mswali yanayoeleweka?
 
Back
Top Bottom