JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Amesema kwamba ni marufuku kwa hospitali zote nchini ambazo zipo chini ya Serikali kuwatoza kuwatoza wananchi pesa ya posho ya dereva wala mtaalamu ambao uhusika kusindikiza mgonjwa na ambulance.
Waziri Ummy ameyasema hayo Julai 28, 2024 akiwa mkoani Tanga wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo, ikiwa gari hiyo kati ya magari 736 yanayodaiwa kununuluwa na Serikali.
Sanjari na hilo Waziri Ummy amesisitiza umuhimu wa matumizi stahiki ya magari hayo huku akionya yasitumike katika shughuli nyingine tofauti ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.