Waziri wa Afya apiga marufuku utumiaji wa shisha Kenya

Waziri wa Afya apiga marufuku utumiaji wa shisha Kenya

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Waziri wa Afya, Cleopha Mailu amepiga marufuku uvutaji na uuzwaji wa shisha sababu ya madhara yake kiafya

Utafiti umeonyesha shisha ina kemikali zaidi ya 200 na ni hatari kuliko sigara

Kwenye tangazo la kisheria lililotolewa tarehe 27 Disemaba, waziri Mailu alipiga marufuku uingizwaji, uzalishaji uuzwaji, matangazo na ugawaji wa bidhaa hiyo

Atakayekiuka agizo hili aatakabiliwa na kifungo cha miezi 6 jela au faini ya Kshs 50,000 au vyote kwa pamaoja, pia kuna faini ya ziada ya Kshs 1000 kila siku

Nchi ya Kenya inakuwa ni ya tatu Afrika Mashariki baada ya Tanzania na Rwanda kupiga marufuku utumiaji wa bidhaa hiyo

Health cabinet secretary Cleopha Mailu has banned water pipe smoking of the flavoured tobacco with immediate effect citing health risks that come with it. Through a legal notice dated 27th December Mailu has equally banned the importation, manufacture, sale, advertisement or distribution of the same product.
 
Unakataza shisha unaruhusu milungi ni sawa kakataza nyama ya ngurue kuliwa ukaruhusu nyama ya ngamia vyote ni haramu mbele za Mungu kuliwa
 
Ona hawa. Sasa mbinu zingine za kuingiza manzi wa Nai box chapchap ndo zitasumbua vichwa vyetu. Dem wa mashisha ilikuwa ni mtelezooo! Can all of the similar opinion say aye! 😀😀😀
 
Serikali ya Kenya imeamua kukopi na kupesiti kasi ya RC Makonda kwenye swala la kupambana na wauza madawa ya kulevya wa ufipa na kupiga marufuku matumizi na uvutaji wa shisha nchini humo.

Shisha na madawa ya kulevya ni hatari kwa afya kwa mtumiaji, hivyo kama kazi ya serikali ni kulinda raia na mali zao basi ni lazima kupiga marufuku mambo yote yanayohatarisha afya za raia.

Kenya sasa ukikamatwa unauza au kutumia shisha utatozwa faini ya dola elfu kumi kila siku.

Hongera Kenya ,hongera RC Makonda ingawa watetea mafisadi (ufipa) hawaoni juhudi zako lakini jumuiya ya kimataifa kama kenya wanakutambua na wameamua kukuiga style zako za kupambana na wahuni.
 
ni jambo zuri kuiga mambo mambo mema kutoka kwa watu wengine.
 
Sio Kenya tu walianza Rwanda kumuiga ndio wakafata wakenya. Ufipa tumbo joto
 
Kuanza mwaka na kusoma stupidi posting !!
Kampeni za kupambana na hizi vitu zipo duniani kote na hata WHO na other onternational health organizations walishatoa angalizo...!
Sasa mtu kuandika eti wamemuiga flan ni kuonyesha matatizo ya ubongo... km ugonjwa wa akina nonino... !

Serikali ya Kenya imeamua kukopi na kupesiti kasi ya RC Makonda kwenye swala la kupambana na wauza madawa ya kulevya wa ufipa na kupiga marufuku matumizi na uvutaji wa shisha nchini humo.

Shisha na madawa ya kulevya ni hatari kwa afya kwa mtumiaji, hivyo kama kazi ya serikali ni kulinda raia na mali zao basi ni lazima kupiga marufuku mambo yote yanayohatarisha afya za raia.

Kenya sasa ukikamatwa unauza au kutumia shisha utatozwa faini ya dola elfu kumi kila siku.

Hongera Kenya ,hongera RC Makonda ingawa watetea mafisadi (ufipa) hawaoni juhudi zako lakini jumuiya ya kimataifa kama kenya wanakutambua na wameamua kukuiga style zako za kupambana na wahuni.
 
Hahaha mbona hata sigara na pombe ni hatari kwa afya ya binadamu hajazizuia?! Alizuia shisha lakini unga upo, mateja wapo,madada poa wapo.
Tulipata faida zipi kwa kuzuia shisha?!
 
Back
Top Bottom