Waziri wa Afya: Epukeni misongamano isiyo ya lazima, vaeni barakoa safi na salama

Na bado mtazunguuka wee mwisho mtarudi kati kuanza upya, sijui tabu yote mnapata ya nini kuzunguuka zunguka wakati kila mwenye akili ukweli anaujuwa.
 
Kuna upuuzi mkubwa sana unafanywa na hii wizara ya afya.

Haiwezekani watengenezaji wengine mpaka wathibitishwe na mfamasia mkuu,wakati uleule wanaruhusu mtu yeyote(binafsi) ajitengenezee barakoa yake mwenyewe.
 
Watu wana mafua makali, wanakohoa sana siku3 4 5 wanapona.

Wengine wanapata shida ya upumuaji yaani mambo mengimengi tuu sana.
Na inaonekana watoto kwa sababu kinga zao ni imara wanaweza kupatwa korona na kupona bila tiba yoyote. So wanaweza kuwa wasambazaji wa korona kwa watu wazima.

Kuna kipindi cha wiki mbili zilizoisha shule fulani mkoani Kilimanjaro wilayani Rombo , shule ya wanafunzi 600 karibia nusu waliugua mafua makali, na kuumwa kichwa, na walipona bila tiba yoyote.
 
JF na nyie mpunguze uoga kupitiliza, nimeandika sijawahi kumuona mkuu wa nchi na huyo waziri wake wa Afya wakiwa wamevaa barakoa inakuwaje wao watake wengine wazivae? nawashangaa mmeifuta comment yangu, kwani kuna shida gani hapo?

Si kiongozi hutakiwa kuongoza kwa mfano, na hili linajulikana popote duniani, sasa kama hao viongozi wetu hawayaishi wanayotamka kwanini wasiambiwe ukweli? wacheni uoga wenu, wasiishie kutuambia sisi tu, wazivae na wao.
 
mwisho wa siku wananchi wameshinda.
 
kila mwaka kipindi cha Novemba hadi Machi wimbi la magonjwa hususan yale yanayoathiri mifumo ya upumuaji na chakula huongezeka. Hii hutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mvua nyingi ambazo huendelea kunyesha kipindi hiki.
Mbona mmeanza kuyasingizia majira badala ya kujilaumu kwa uzembe wenu
 
Coroooo.. corona🎼 mama.. corooo corona🎶 embe doodo embe dodo🪕 tutafika tu, neno corona limekua zito kuliko mfuko wa cement
 

Mnachukua hatua gani za kulazimisha utii kwa watu wanaolazimisha misongamano kama vyombo vya usafiri means mabasi na hasa mwendo kasi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…